@kusagatv: MWENYEKITI UVCCM PWANI AMVAA MCHENGERWA, ATOA WITO WA KUOMBA RADHI Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Pwani, Samaha Seif Said, amekemea vikali kauli ya Waziri wa Afya na Mbunge wa Jimbo la Rufiji, Mohamed Mchengerwa, akidai kuwa imewadhalilisha na kuwakatisha tamaa vijana wanaojitolea kukitumikia chama hicho. Samaha amesema kauli ya Mchengerwa, aliyesema vijana hawafanyi kazi bila kupewa hongo na kwamba wamechagua upande, si njema kwa vijana wa UVCCM, huku akieleza kuwa wako tayari hata kuomba Radhi endapo itabainika wamemkosea lakini Kwa makubaliano ya Kistaarabu na Maslahi ya Umoja kuliko kuziachia kauli zake kama ambavyo amefanya . Akizungumza kuhusu kauli hiyo iliyotolewa na Mchengerwa mjini Kibaha wakati akifungua kikao cha Baraza la UWT Mkoa wa Pwani, Samaha amesema kauli hiyo imewaumiza vijana na kuhoji sababu za kuwahusisha na rushwa wakati si kipindi cha uchaguzi. “Kauli hii imeniuma na si njema kwa vijana. Kama kuna sehemu tumekosea, Mchengerwa ana nafasi ya kutuita na kutueleza, nasi tuko tayari kumuomba radhi kama tumemkosea. Lakini kwa nini anasema vijana wamechagua upande na kuwaita wala rushwa? Je, ni kweli hatufanyi kazi bila rushwa?” amehoji Samaha. Aidha, Samaha amemtaka Mchengerwa kutaja wazi mtu au watu anaowalenga ikiwa ana malalamiko binafsi, badala ya kutumia kauli zinazoweza kuchafua taswira ya jumuiya nzima, akisisitiza kuwa vijana wa UVCCM wanajitolea kwa ajili ya chama na hawapaswi kudharauliwa.

MWANDISHI WA WANANCHI
MWANDISHI WA WANANCHI
Open In TikTok:
Region: TZ
Saturday 17 October 2026 17:32:37 GMT
38850
552
70
49

Music

Download

Comments

fatwima
FATKONDO :
Kinachotumika hapaaa sio maadili yaa chama cha MAPINDUZI ukiwa mw/kiti wa k/utekelezaji uvccm mkoa mw/kiti wa baraza la uvccm mkoa na mjumbe wa k/siasa unayo nafasi ya kuzungumza kwenye kikao Pwani. Sio kuongea kwny media.
2026-10-18 13:52:08
2
geraldjabu1.com
Gerald Jabu1 :
Ukweli mchungu ila hii taarifa wala haitasambaa kama wale wa kumkataa Heche 😁😁😁
2026-10-17 20:03:37
5
awadhmagulio
awadhmagulio :
rapid downfall ....
2026-10-18 01:14:02
2
raphaelmalima6
raphaelmalima6 :
povu la nn mdogo wangu Mchengerwa ameongea yaliyopo na hajamtaja mtu jina awaite il iweje
2026-10-19 04:30:11
2
ostacknazia4
ostacknazia576 :
kwani alivyozungumzia rushwa ni vibaya jamani?
2026-10-18 15:16:57
3
mwinyimvuamsabaha
Mwinyimvua :
Shida ipo kwa Vijana, tafuteni ufumbuzi wa kile kilicho semwa, Kiongozi unapaswa kupokea taarifa kisha chunguza na kufanyia kazi.
2026-10-19 18:05:10
1
eng.mwafyijinja
Mwafyijinja_🐵 🤨 :
Distraction well planned 🥺😏
2026-10-18 16:35:37
1
user36122481494364
[email protected] :
mchengerwa yupo sahihi 💯 na ndo ukweli...vijana hawatoki kwenye vikao pesa. ..ukiwambia mkutano wanauliza Kuna hela??
2026-10-20 02:32:08
1
edwinitematema
Edwini Tematema :
98%ya uongozi wa ccn bila rushwa hupati uongozi.hata yy kuna siku alifanya hivo hiyo ndo ccm amesema ukweli ndo ccm ilvyo
2026-10-18 17:18:27
1
user2313908887808
user2313908887808 :
unakataaje kama vijana wenzio wanao ambiawa wanashangilia ujumbe huo konesha kuwa kinachosemwa ni kweli.
2026-10-18 11:03:25
3
meck.kkifuka
MECK KKIFUKA :
Mtafanya nini
2026-10-20 14:08:15
0
user6386835467207
malale.lazima :
mkome mmezidi rwiswa 👍 safa kaka 🙏🇹🇿 Tanzania
2026-10-20 15:31:18
0
maytham6537
maytham :
Nikweli anaongea kwanini asiseme kweli
2026-10-19 19:04:59
0
user14527248
Mc Hellen Mbunge :
Vijana mnatumia NGUVU nyingi kujitetea.
2026-10-19 22:18:49
0
edwinmrema
EDWIN MREMA :
Maisha yana mengi
2026-10-17 20:17:08
0
yaseenmohammed846
YAS££N🇹🇿 :
Kuongea nnje ya vikao ni kinyume na taratibu za maadili,kulalamika pembeni unakosea dada yangu,
2026-10-18 04:51:14
0
user36122481494364
[email protected] :
sahihi kabisa mkuu
2026-10-20 02:29:58
0
user36122481494364
[email protected] :
ndo ukweli mkuu siyo uongo?? na umenyokaa sanaa
2026-10-20 02:30:34
0
mwamnyange2
Mwamnyange 🇹🇿 🇨🇦 :
Fanyeni kazi
2026-10-19 14:30:16
0
elmlawatu957
mlawatu :
ni kwel hamfanyi ktu bila rushwaa ,rushwaaa rushwaaa
2026-10-19 12:21:57
0
user3723786956234
mwajuma kashoka :
hampendi kuambiwa mmezidii
2026-10-20 18:43:14
0
user4297668384814
Dr changale :
Sasa mnamuomba radhi yy au wananchi
2026-10-19 18:29:28
0
barakamallo
barakamallo :
Uvcc vinapenda Rishwa mnoo! Mmeammbiwa ukweli Vijana wa CCM fanyeni kazii
2026-10-19 14:19:13
0
user9186927958754
Horoma Fidel :
vijana amkeni siasa za sasa haziheshm..utu.
2026-10-19 12:50:49
0
user5453650263946
mwanakhamis @mzula :
vijana kubalini ukweli
2026-10-17 21:28:51
0
To see more videos from user @kusagatv, please go to the Tikwm homepage.

Other Videos


About