@bongo_media: Mwadada amewakosoa baadhi ya wanawake kwa kile alichodai kuwa wanajikita zaidi katika kuzungumzia na kulaumu tabia za wanaume kuchepuka, huku wakisahau wajibu wao katika kuwajali na kuwahudumia waume zao. Amesema kuwa mwanaume anapojitahidi kumhudumia mke wake, kumjengea nyumba na kuhakikisha anapata mahitaji muhimu, mwanamke naye anapaswa kuonyesha upendo, kujali na kumhudumia mwenzi wake. Aidha, amesisitiza kuwa uhusiano wa ndoa unahitaji juhudi kutoka pande zote mbili, akiwataka wanawake kutafakari namna wanavyowatendea waume zao badala ya kuangalia makosa yao pekee.