@sammyrah__: Hutapata katika dunia hii mwenza aliekamilika au maisha yaliyokamilika, kwa sababu ukamilifu sio sifa ya hii dunia. Tunachotakiwa ni kurekebisha tunapoweza, kuvumilia pale inapobidi, na kusamehe makosa na madhaifu ya wengine. "Na wasamehe na waachilie. Je, hamtaki Allah awasamehe?" — Qur'an 24:22