@afmradiotz: Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma, kupitia operesheni za ukaguzi wa vyombo vya moto, limeendelea kuchukua hatua kuhakikisha usalama wa abiria na watumiaji wengine wa barabara unazingatiwa. Katika operesheni hiyo, Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Dodoma, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) Yusuph Kamotta, alifanikiwa kulisimamisha basi la kampuni ya katarama luxury lililokuwa limezidisha idadi ya abiria wanaoruhusiwa kusafiri. Miongoni mwa abiria waliokuwamo ndani ya basi hilo ni mwanafunzi anayetarajiwa kuanza mwaka wa kwanza chuoni, aliyekuwa akisafiri kutoka Bukoba kuelekea Dar es Salaam kwa ajili ya kuanza safari yake ya elimu ya juu. Inadaiwa kuwa mwanafunzi huyo alilipa nauli ya shilingi 110,000 kwa safari yake, lakini licha ya kulipa kiasi hicho, alilazimika kukaa chini katika sehemu ya basi hilo kuanzia Bukoba hadi alipofika Dodoma, kutokana na kuzidi kwa idadi ya abiria. Hata hivyo, hali hiyo ilibainika wakati wa ukaguzi uliofanywa na Kamanda Kamotta, ambaye baada ya kubaini changamoto iliyomkabili mwanafunzi huyo, alimuagiza kondakta wa basi hilo kumrejeshea fedha zake ili aweze kutafuta usafiri mwingine na kuendelea na safari yake katika mazingira salama. Hatua hiyo inalenga kusisitiza umuhimu wa wamiliki wa mabasi, madereva na makondakta kuzingatia sheria za usafirishaji, ikiwemo kubeba idadi ya abiria inayoruhusiwa na kuhakikisha kila abiria anapata nafasi inayostahili kwa usalama wake. #10YearsOfAFM #Miaka10YaAFM #VibesKubwaTOFAUTI

Afmradiotz
Afmradiotz
Open In TikTok:
Region: TZ
Sunday 18 October 2026 03:32:03 GMT
399972
40488
3437
1364

Music

Download

Comments

mpn.jmp.kivuluge
MPN JMP KIVULUGE MTY2 :
police yupo sahihi wakuu au mnasemaje watanzania
2026-10-18 05:01:38
3741
pierresamweri
Merryline :
ubarikiwe baba[Red heart][Red heart][Red heart]
2026-10-18 08:46:12
0
mkaka17
M K A KA _17 👑 :
Ila first year wanapitia mengi😂😂
2026-10-18 06:45:38
473
user6093453600446
lucmon200🥰 :
laki na elf 10 ni kutoka mkoa gani jmb
2026-10-18 05:11:31
517
francisaurelian9
Francis :
Huyu Askari Abarikiwe sana
2026-10-18 05:52:50
642
gervassemgabo
Hekaheka :
Huyu afande abarikiwe sana aiseeeh
2026-10-18 05:03:31
2534
nhulila1
nyau mpolloo :
kazi nzuri sana. napenda sana askari kama huyu
2026-10-18 04:41:46
1701
nyakunga_boy
Isaya_nyakunga :
Hongera kwa Jeshi la Polisi Tanzania Kazi nzuri🥰🥰🥰
2026-10-18 04:46:31
702
annatillya
My Annie❤️❤️ :
Inaumiza sana kumbe amelipa nauli yote😭
2026-10-18 05:10:00
923
peki213
peki :
Polisi apewe mauwa yake
2026-10-18 05:03:58
152
joh_boy01
💥Hillu 📌Khan💥 :
Sasa police ndo wanatakiwa kuwa wema kama hivi😁😁😁😁
2026-10-18 05:17:57
345
flaziam
flaziam :
wewe sio Asikari tu wewe ni baba mzazi Mungu akuweke hongera sana
2026-10-18 06:31:46
254
elizabethcharles248
Elizabeth Charles :
apewe mauwa yake
2026-10-18 08:49:48
0
yohanathefrench
yohana the french guide. :
police apo umefanya kazi nzuri
2026-10-18 04:54:14
290
teresiaamosiqamri
Teddy Amos :
yaan nawapenda sana maaskari na naomba waendelee na huo moyo
2026-10-18 05:08:10
172
lema.leis
Lema Leis :
Elfu 50 ya TZ ni hela ngpi za Kenya?
2026-10-18 05:34:07
35
swai584
Black beauty ❤️ :
Makofi kwa police
2026-10-18 06:18:59
2
eze_hd4k
🪖HD 4k ✊🏾 :
ila first year 🙌🏾🙌🏾🙌🏾🙌🏾🤣🤣
2026-10-18 08:01:24
1
rosetenga0312
rosetenga😍 :
AFANDE UKO VIZURI SANA🥰🥰
2026-10-18 05:08:59
63
peterjoseph7230
Great joseph :
kumbe nao police wanaroho nzuri , hongera sana mkuu
2026-10-18 05:20:25
63
josephmsaky4
ven,chesco. :
abiria mwenyewe anatamani afike dar😂😂
2026-10-18 05:06:59
390
fashiondesigner142
happiness :
nimempenda huyu askari
2026-10-18 05:52:22
97
001xtwnk
Lly 01 :
Kila la kheri first year mwenyew ni mpole anaonkn
2026-10-18 06:10:53
80
mwombeki77
Mwombeki :
Kwenye hili nakupongeza kamanda
2026-10-18 05:06:43
54
mjema9999
Drone mwanza Nax :
Nimependa hii kimsingi busara angepakiliwa bure
2026-10-18 04:53:45
195
To see more videos from user @afmradiotz, please go to the Tikwm homepage.

Other Videos


About