@kiswahilitvonline: "Prisoner" wimbo wa Lucky Dube uliotolewa mwaka 1989, wakati huo Afrika Kusini ilikuwa bado chini ya mfumo wa apartheid, uliowabagua watu kwa misingi ya rangi. Katika wimbo huu Lucky Dube, alikuwa akimuelezea mhusika katika wimbo ambaye alishauriwa akiwa mtoto kwamba uhalifu haulipi na elimu ndiyo ufunguo. Lakini hakusikiliza ushauri huo, mwishoe akajikuta gerezani, lakini pia alitumia nafasi hiyo kuikosoa jamii inayowekeza zaidi katika kuwaadhibu watu baada ya kufanya makosa kuliko kuwekeza katika elimu inayoweza kuwasaidia kuepuka makosa hayo. 📌Jamii inayowafungia watu bila kushughulikia matatizo yanayowasukuma kwenye uhalifu inaweza kuwa inatibu matokeo badala ya chanzo. Wakati mwingine minyororo mikubwa zaidi haionekani kwa macho. 🕊️🌍
some body told me about when I was still a little boy he said to me clime doesn't pay he said to me education is a key as a little I thought I I know was goog but today I am in jail I am a prisoner