@jambotv_: VIDEO: Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Njombe kupitia CHAUMMA, Sigrada Mligo, amesema wananchi wa mkoa huo wamekuwa wakilalamikia hali ya barabara kwa zaidi ya miaka 25, huku ahadi za kuziboresha zikiendelea kutolewa katika Ilani ya CCM kila mwaka bila kutekelezwa. Malalamiko hayo yamekuja wakati Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Deogratius Ndejembi, akimtaka Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Masanja Kadogosa, kuchukua hatua za haraka dhidi ya mkandarasi anayejenga barabara ya Itoni–Lusitu yenye urefu wa kilomita 50 kwa kiwango cha zege, inayogharimu zaidi ya Sh bilioni 120. Akizungumza na wananchi wa Halmashauri ya Mji wa Makambako, mkoani Njombe, Oktoba 17, 2026, Ndejembi amesisitiza kuwa watendaji wa Serikali wanapaswa kuwasimamia kwa karibu wakandarasi wanaotekeleza miradi ya maendeleo badala ya kusubiri viongozi wa juu kuingilia kati. “Fedha za Watanzania zipo, zimeshakuja. Mnatakiwa kuwasimamia wakandarasi, tusisubiri kumbembeleza mkandarasi. Yeye ni muajiriwa, ameajiriwa na TANROADS kwa niaba ya Serikali. Tunapaswa kumsimamia; haikupaswa waziri amuite Dodoma wakati fedha ameshalipwa,” amesema Ndejembi. Kwa upande wake, Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Masanja Kadogosa, amesema mkandarasi huyo tayari amelipwa Sh bilioni 14 kama fedha za awali, hivyo anapaswa kutekeleza mradi huo kwa kuzingatia masharti ya mkataba.

Jambo TV
Jambo TV
Open In TikTok:
Region: TZ
Sunday 18 October 2026 07:41:17 GMT
75075
2381
82
67

Music

Download

Comments

mussabakari21
mussabakari21 :
dahhh huyu dada ana kitu
2026-10-18 08:24:32
23
user3234365986556
Wonder VG :
appreciated 👏 💐
2026-10-18 15:30:58
0
wazir.tz
WAZIR🇹🇿 :
aliyekua kwenye hicho cheo muda wote alikua anataka katiba mpya, Mwamba anapambania taifa Kila kukicha, Piga kazi Mkuu.
2026-10-18 09:34:56
15
user2447847819253
Max :
nice statement sigrada
2026-10-18 09:00:28
0
elizabethkawogo2
Elizabeth Kawogo :
sgirada mligo ni mmoja tu
2026-10-18 09:16:05
20
efm_store
EFM_STORE :
This woman😂😂
2026-10-18 12:29:03
1
user8722512466383
user8722512466383 :
huyu mbunge namkubali
2026-10-18 09:01:31
5
victoria.nduva
Victoria Nduva :
semligo hongera Sanaa na ww umeongea kimamlaka umetumia mda mchache sana ila umeongea poind mm SI wa njombe ila umenifrahidha sana
2026-10-18 12:31:03
2
marera.expedition8
marera expedition :
hii ndo Tanzania tulioimisi Kwa muda murefu kwamba siasa sio uadui na kutofautiana mtazamo si dhambi lengo ni moja tu nikujenga nchi yetu .hakika jicho la raisi wetu iliona vema Kwa Deo
2026-10-18 12:32:20
2
user8837538178195
mom g :
njombe lupila umetusahau
2026-10-18 11:14:51
1
ginimbi.tz
Ginimbitz :
2030 Kura za maoni Mtifuano mkali sana huku Mwigulu huku Makonda huku Ndejembi, Gaza kule Ummy, Kairuki,Wanu
2026-10-18 09:40:43
3
home.of.cosmetics
Home of Cosmetics :
kunajambo lipo nyuma juu ya haya yanayoendelea
2026-10-18 10:19:03
4
adammuki696
muki :
kwa nn mnampa kazi nyingi yy peke yk uo si mchongo uo
2026-10-18 09:58:15
1
kiaziobama
VIAZI ONLINE 🙈🙈 :
kama sigrada amemkubari basi namimi nimemkubari😂😂
2026-10-18 11:47:06
1
cocoboy686
mbusye :
makamu wa Rais kakubalika na mbunge Sigrada
2026-10-18 13:19:20
2
rehema.mligo4
Rehema Mligo :
sigrada mligo
2026-10-18 10:58:45
1
allyurembo735
Ally Urembo :
kwa mama ametuchagulia mtu kweli kweli namkubali sana huyu makamu mtu mmoja mipiga kazi kweli kweli mungu amusement sana
2026-10-18 09:11:41
3
user23109734271678
Robby dhe don :
safi sana mbunge wetu
2026-10-18 11:13:30
1
ushindi_edson
@Ushindi Edson :
Mi huwa napenda viongozi ambao hawaogopi kusikia hoja hata zinazo wachallange, hilo linaprove kuwa IQ yake iko vizuri.
2026-10-18 13:00:20
1
stanleympangala88
StanleyMpangala :
Aje Ndachi kata ya Mnadani uku Dodoma changamoto ya ardhi , barabara ni shida sana
2026-10-18 10:30:27
1
octavian_kangalawe
octavian_kangalawe :
mtoto wa mwenyekiti wa ccm mkoa enzi izo ni mpambanaji mwenzetu?
2026-10-18 09:15:10
3
buthaynah40
Buthaynah :
Yaani hii siasa naipenda sana tuwe hivi😂
2026-10-18 10:43:11
1
rubenlugaganya
Ruben Lugaganya :
Utadhani wanaotawala ni wapinzani kumbe wao wenyewe toka uhuru halafu wanalalamikiana wenyewe 😂
2026-10-18 11:54:27
1
t.370.zip
Quality Brother :
kwani mh mwenyewe yupo jamani mbona hapigi hiz mbungi za mtaa kwa mtaa??
2026-10-18 09:31:09
0
givenilomo
#sosoli jr :
huyu wangekua na maghufuli nchi ingekwenda haraka
2026-10-18 09:43:55
1
To see more videos from user @jambotv_, please go to the Tikwm homepage.

Other Videos


About