@kishkionlinetv: Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, amedai kuwa Iran inatengeneza makombora ya masafa marefu ya balestiki (ICBM) yenye uwezo wa kubeba vichwa vya nyuklia na kufikia Marekani. Netanyahu ameonya kuwa endapo Iran itafanikiwa kupata uwezo huo, miji yote ya Marekani inaweza kuwa katika hatari ya kushikiliwa kama mateka kupitia tishio la mashambulizi ya nyuklia. “Kila mji mmoja nchini Marekani utashikiliwa kama mateka,” Netanyahu amesema, akieleza ukubwa wa tishio analodai linaweza kujitokeza. ________________________ Tufuatilie KISHKI ONLINE TV kwenye: Instagram → KISHKI ONLINE TV Facebook → KISHKI ONLINE TV TikTok → KISHKI ONLINE TV ▶️ YouTube → KISHKI ONLINE TV #mtazamo #KishkionlineTv #nuruyadiniyako