@wendefm: Maji ya Baraka ni miongoni mwa vivutio vinavyopatikana katika Hifadhi ya Mpanga Kipengere, mkoani Njombe, ambayo yanatajwa kuwa na umuhimu katika masuala mbalimbali ya maisha, yakiwemo mafanikio ya kiuchumi, ustawi wa familia na mahusiano ya kimapenzi. Akielezea kuhusu kivutio hicho mwongoza watalii katika hifadhi hiyo, Leonard Nsajigwa, anasema maji hayo yanahusishwa na imani mbalimbali za jamii kuhusu namna yanavyoweza kutumika katika maisha ya kila siku. Akitolea mfano Nsajigwa amesema wanawake wanaweza kutumia maji hayo wakati wa kufua nguo za waume zao kunaweza kusaidia kuimarisha mahusiano ya kimapenzi. #nguvuyaupendo❤️🤍 #wendefm