@licado.page: Barabara Kuu ya Segera–Tanga itafungwa kwa muda wa saa nne kesho, Oktoba 20, 2026, kuanzia saa 2:00 asubuhi hadi saa 6:00 mchana, ili kuruhusu matengenezo ya madaraja ya Hale na Maguzoni. Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), Mkoa wa Tanga, Msama Kosani, amesema matengenezo hayo ni mwendelezo wa kazi zilizofanyika awali katika sehemu za chini za madaraja hayo, ambapo kwa sasa ukarabati utafanyika katika sehemu za juu ili kuimarisha usalama wa watumiaji wa barabara hiyo. Kosani amewataka watumiaji wa barabara hiyo kuwa wavumilivu wakati wa utekelezaji wa zoezi hilo, akieleza kuwa maandalizi ya vifaa yamekamilika ili kuhakikisha kazi zinafanyika kwa haraka na huduma za usafiri zinaendelea mara baada ya matengenezo kukamilika. Ameongeza kuwa hatua hiyo ni sehemu ya mkakati wa kuimarisha madaraja na kujiandaa kukabiliana na athari za mvua za El Niño zinazotarajiwa kunyesha kabla ya Desemba. Watumiaji wa barabara hiyo wanashauriwa kupanga safari zao mapema ili kuepuka usumbufu. #LicadoPage #licadoupdats
Licado Page
Region: TZ
Monday 19 October 2026 06:13:30 GMT
Music
Download
Comments
Rich♥️ aunt :
[Innocent][Innocent][Innocent][Innocent][Innocent]khaaaa jamani
2026-10-19 09:04:30
0
wazumikacho :
tonight device rod
2026-10-19 09:32:32
0
SALIMU CHALULA :
tafuteni njia mbadala hiyo barabara ni kubwa sana kwa masaa manne mtawapa watu shida
2026-10-19 07:43:32
9
Sheim_tz•Hikmah :
unayajua masaa manne ya bongo
2026-10-19 08:10:54
1
Mangi05 :
hiv hay masaa ma4 kwanini yasiwe yausiku maana matumizi nimadogo kuluko hy asubuhi
2026-10-19 08:22:44
4
sule talent48 :
alf tutapita wap
2026-10-19 07:46:00
1
Sato :
tengenezeni njia mbadala, acheni janja janja
2026-10-19 07:50:10
3
Mahuja Jr :
hilo daraja la hale sio la kutengeneza masaa 3 kama huamini kasimame pemben alafu gar la mzigo lipite daraja linanesa sana hilo bila kulifumua kuanza upya kuna siku litaleta tukio baya
2026-10-19 08:57:05
1
mohamediomari5 :
Tanzania hatuna wataalamu yaani mnafunga uchumi wa mkoa bila kujiandaa kuweka madaraja ya dharura,kwann hiyo kazi usifanye usiku
2026-10-19 08:20:08
0
Gembe mo :
hayo ni masaa 6 na sio 4
2026-10-19 10:26:45
0
Beka Tz🙏 :
kama mpango upo muda mrefu tengenezeni madaraja ya dharula ili nanyinyi mpate muda mzuri wa kutengeneza
2026-10-19 07:58:15
0
hemedi Abedi :
sasa kwa nini musi kwangue hata rafu rodi pembeni tukaendelea kupita kwa muda
2026-10-19 10:32:26
0
SASHA RYAN :
kwa nini msifunge usiku saa sita mpk saa 12 asbh
2026-10-19 10:43:21
0
Mussa official :
hongera sana bossi wangu ulinilea kwa upendo
2026-10-19 09:33:52
0
Abel Munis :
huo ni uzembe wa akili mngeejenga daraja jingine pembeni ili wasaafiri wasipoteze mdaa wao,
2026-10-19 10:07:01
0
Smart Generation 🍿 :
Basi nitapanda ndege DSM to Arusha chap tu.... ahsante kwa taarifa mkubwa 🙏
2026-10-19 10:20:42
0
Ivan :
Sisi bado sanaaaaaaaa... kwanini msifaye kuanzia saa 8 hadi saa 11 asubuhi?
2026-10-19 10:02:08
0
mohamediomari5 :
tafuteni mbadala wa jambo hilo acheni kukurupuka maana kufunga uchumi wa TANGA mjini
2026-10-19 10:07:15
0
shayhan & shayhan :
hiii nchi ina viongozi wa Ajabu sana
2026-10-19 08:10:07
0
Athuman kp :
kuweni wakweli tu hapo sio masaa 4 ni siku nzima
2026-10-19 11:08:54
0
rajabutingisha677 :
sasa kwanini msijenge usiku kuaza saa 8 usiku adi 12
2026-10-19 10:44:16
0
Pety Marck :
Tafuteni daraja la muda kwanza
2026-10-19 09:51:06
0
@Ramso J Tz2 :
fanyen usiku
2026-10-19 09:43:57
0
user6835242800410 :
Kwa siku ngapi?
2026-10-19 09:25:58
0
Devis ndosi :
noma sanaa
2026-10-19 07:42:45
0
To see more videos from user @licado.page, please go to the Tikwm
homepage.