@football.moments0296: Fikiria mnaipiga timu pinzani mvua ya mabao 4-1 halafu kwenye moja ya jukwaa la VIP la uwanja yupo Vinicius Junior akiwa ametulia anatazama. Wakati watu wengi wakisema kuwa kukosekana kwa Vinicius kungeigharimu na kuiletea uzito Real Madrid, wakatokea wachezaji kama Yan Diomandé, Kylian Mbappé, Jude Bellingham na Arda Güler wakashusha burudani na ufundi wa kiwango cha juu uwanjani. Hayo yote yanatokea huku Vinicius akiwa kwenye jukwaa la Santiago Bernabéu akipata burudani. Bado hatujapima wala kuelewa ukubwa wa kipaji na uwezo uliojaa kwenye kikosi hiki. Halafu benchi yupo gwiji kama José Mourinho. Kwa faida ya soka, bado hata hawajaonyesha kiwango chao cha juu kabisa. Hatujajiandaa kwa kile kinachokuja Hizo ni starehe na jeuri anazoweza kujipa The Special One pekee!