@breezt4: SISTER THEODORA FAUSTIN AWATAKA WAZAZI KUWALEA WATOTO KATIKA UTAMADUNI WA HISANI NA KUJALI WENYE UHITAJI Sister Theodora Faustin, Mkuu wa Shule ya Sekondari ya St. Joseph Cathedral High School, ametoa wito kwa wazazi na walimu kuwalea watoto katika misingi ya huruma, ukarimu na kuwajali watu wenye uhitaji, akisisitiza kuwa watoto wanapaswa kujifunza kushirikiana na wenzao wenye changamoto za maisha tangu wakiwa wadogo. Akizungumza wakati wa Matembezi ya Hisani, maarufu kama Charity Day, Sister Theodora amesema watoto wanaolelewa katika familia zenye uwezo wa kiuchumi wanapaswa kufundishwa kutambua kuwa si kila mtoto ana nafasi sawa ya kupata mahitaji muhimu kama chakula, mavazi na makazi. Amesema ni wajibu wa wazazi kutumia mazingira ya kila siku kuwaelimisha watoto kuhusu changamoto zinazowakabili watu wengine katika jamii, ili kuwajengea moyo wa huruma na utayari wa kushiriki kile walicho nacho na wenye uhitaji. Aidha, ameeleza kuwa shule za Kanisa zina utaratibu wa kuwasaidia wanafunzi kutoka familia zenye changamoto za kiuchumi kupata elimu kupitia ufadhili wa majimbo na wafadhili mbalimbali. Amesisitiza kuwa shule hizo pia huweka msisitizo katika usawa wa wanafunzi kwa kuhakikisha tofauti za kiuchumi hazisababishi baadhi yao kujiona duni mbele ya wenzao. Sister Theodora amebainisha kuwa malezi ya kiroho na kijamii ni muhimu katika kumjenga mtoto mwenye utu, akisisitiza kuwa thamani ya mtu haipimwi kwa mali alizonazo, bali kwa tabia yake, utu na namna anavyowatendea wengine. Amehitimisha kwa kutoa wito kwa wazazi na jamii kwa ujumla kushirikiana katika kuwalea watoto wanaotambua umuhimu wa kutoa, kusaidia na kuwajali wengine, akisisitiza kuwa malezi bora yanapaswa kumfundisha mtoto si tu kupokea, bali pia kushiriki alicho nacho kwa ajili ya ustawi wa wengine. Imeandikwa na Izahaki Mwacha #KanisaKatoliki #mkombozicommercialbank #Tanzania #BaloziwaAmani #breezonlinetv #woisooriginalproducts #CharityDay #news

Breez Online Tv
Breez Online Tv
Open In TikTok:
Region: TZ
Monday 19 October 2026 13:08:55 GMT
9680
385
21
41

Music

Download

Comments

edna.msele
Edna Msele :
kweli kabisa sister
2026-10-19 16:05:10
5
user1608029403203
Vin dezel :
Hii ndio maana ya elimu
2026-10-19 18:08:31
4
user6009561270112
user6009561270112 :
Asante sana Sista kwa ushauri. Kwa kweli mnafundisha, mnalea. Nawashukiruni mno masista...
2026-10-19 16:31:33
4
braynernyenzakipenzchaw1
kipenzi cha watu muhehe :
kwely
2026-10-19 19:06:52
2
paulo.mashauli1
Paulo Mashauli :
nikweli. sista
2026-10-19 16:39:29
2
godfre164
Godfrey used spare parts :
real
2026-10-19 13:30:49
2
michaelfesto465
Ozonë :
sikia marioooo uko
2026-10-19 21:03:12
1
juliusfrancetarimo900
Surveyor Tarimo :
point sana hyo
2026-10-19 18:46:10
3
nataliamrosso2
norbertnatalia................ :
sawa kabisa
2026-10-19 16:09:19
3
nillan750
genuithe❤️ :
bravo
2026-10-19 17:04:38
2
magrethmayamba
Magreth Mayamba :
nikweli
2026-10-19 13:27:39
2
goodluck.swale5
Goodluck Swale💕😒😘♻️ :
sister niambie sanamu yako nijenge Roma Vatican 🇻🇦 au dar es Salaam
2026-10-19 19:46:20
1
benmhone
Ben :
wanasema me nimeishi kwa shida sana wanangu hawatoishi hvo, kumbe tunatengeneza bomu
2026-10-19 22:03:50
0
megavision.eye.clinic
megavision.eye.clinic :
🙏🙏
2026-10-19 16:08:44
1
laurent.pius2
Laurent Pius :
🙏🙏
2026-10-19 14:01:33
1
its__nems
its nems boy :
mwambie mwanao kuna kukosa . ili siku akikosa ajue kupambana asitafute shortcut .key point 🙏🏾
2026-10-19 22:17:51
0
mr_victony001
Mr_victony :
yaan sisi shule yetu ulikuw huruhusiw kukaa na pesa na duka hakuna linauza tu madafar wote mnakula chakula cha shule
2026-10-19 18:37:25
2
emmanuel.msodoki0
emmanuel msodoki :
proud to be Catholic!!! hatunaga mazuzu sisi
2026-10-19 17:58:05
3
alex.sichone4
Alex Sichone :
hii ndo Rumi
2026-10-19 16:53:16
2
user5326632261446
user5326632261446 :
🙏🙏🙏
2026-10-19 16:15:36
2
To see more videos from user @breezt4, please go to the Tikwm homepage.

Other Videos


About