@dunialeo_: Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi, amesisitiza umuhimu wa mawazo bunifu ya vijana katika kukuza biashara, kutengeneza ajira na kupanua wigo wa masoko ndani na nje ya Afrika Mashariki. Ujumbe huo umetawala ufunguzi wa Kongamano la Wiki ya Biashara Bunifu Tanzania 2026, lililofunguliwa leo, Oktoba 19, 2026, katika Ukumbi wa JNICC jijini Dar es Salaam. Katika kongamano hilo, msisitizo umewekwa kwenye uwezo wa mawazo yanayozaliwa kwa vijana wa Kitanzania kubadilika na kuwa kampuni kubwa zinazoweza kuajiri mamia ya watu na kuhudumia masoko ya Afrika Mashariki na maeneo mengine duniani.#dunialeoUPDATES
DuniaLeo
Region: TZ
Monday 19 October 2026 17:28:22 GMT
Music
Download
Comments
There are no more comments for this video.
To see more videos from user @dunialeo_, please go to the Tikwm
homepage.