@jamesatilio: Kuweka malengo kwa kuyaandika Kunaweza kubadilisha maisha yako! Amua unataka nini, kisha kiandike. Zoezi la kuandika malengo yako lina nguvu kubwa sana kuliko unavyofikiri. Narudia tena.... Amua unataka nini na uandike kwenye karatasi. Yatoe mambo kichwani yaweke chini kwenye karatasi ili uyaone vizuri. Tengeneza orodha ya mambo unayotaka kufanikisha katika maisha yako. Unataka kwenda wapi? Unataka kufanya nini? Unataka kuona nini? Unataka kuwa mtu wa aina gani? Unataka kuwa na nini? Unataka kushirikiana na wengine katika mambo gani? Ungependa kusaidia au kufadhili miradi gani? Ungependa watu wakukumbuke kwa jambo gani? Ni ujuzi gani ungependa kujifunza? Ni mambo gani ya kipekee ambayo ungependa kufanya katika maisha yako? Ni mambo gani ya kawaida ambayo ungependa kufanya? Na hata kama ni mambo madogo, ambayo wengine wanaweza kuyaona kuwa ya kipuuzi, lakini wewe ungependa kuyafanya? andika yote Vilevile, ni mambo gani muhimu sana ambayo unatamani kuyatimiza? Amua kuhusu mambo hayo yote unayoyataka, kisha yaandike. Kasome Habakuki 2:2-3 Usiandike malengo yako kisha uyaache tu bila kuwa unayaangalia mara kwa mara. Yaweke mahali ambapo unaweza kuyasoma na kuyafanyia tathmini mara kwa mara. Kwa kufanya hivyo, orodha yako itakuwa kumbukumbu ya safari yako ya maisha, ikikuonyesha ulipoanzia, umbali uliotoka na jinsi unavyoendelea kukua na kubadilika. Kadiri unavyojifunza na kukua, ndivyo mtazamo wako kuhusu maisha unavyoweza kupanuka. Unaweza kuanza kuona fursa ambazo hapo awali hukuziona, kutambua mambo ambayo hukuyapa umuhimu, na kugundua mambo mapya unayotamani kuyafanikisha. Hiyo ndiyo nguvu ya kuweka malengo. Malengo yanakusaidia kutambua unachotaka, kufuatilia ukuaji wako na kuendelea kujenga maisha yenye mwelekeo. Nimeandika ebook za kutosha kuhusu uwekaji wa maelngo, unaweza kutumia namba hizi kuwasiliana 0759 551 270 N asiku zote kumbuka Lolote lile utakalo liamini basi lLINAWEZEKANA kama tu Utaamua kuchukua HATUA. INAWEZEKANA!
James Atilio
Region: TZ
Wednesday 21 October 2026 05:31:57 GMT
Music
Download
Comments
BUSINESS MENTORSHIP :
Truth fam 🤟🏿
2026-10-21 18:27:52
0
Zawadi chusi :
Asante
2026-10-21 16:23:17
0
Abubaa Mayai :
Thank you
2026-10-21 08:21:25
0
Emmanueli ndalu :
asantee
2026-10-21 06:26:03
0
To see more videos from user @jamesatilio, please go to the Tikwm
homepage.