@rashidbattashy: WATUHUMIWA TISA WAKAMATWA KWA TUHUMA ZA KUHUSIKA NA MAUAJI YA MWANAFUNZI PEMBA ✍🏻 @rashidbattashy Jeshi la Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba limewakamata watuhumiwa tisa kwa tuhuma za kuhusika na mauaji ya mwanafunzi Raiyan Hemed Amour, mwenye umri wa miaka 15, aliyefariki Oktoba 2, 2026, huku uchunguzi wa tukio hilo ukiendelea. Akitoa taarifa hiyo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi William Mwampaghale, amesema tukio hilo lilitokea katika Kijiji cha Kwale Mpona, Shehia ya Finya, Wilaya ya Wete, Mkoa wa Kaskazini Pemba. Amesema mwanafunzi huyo alifariki baada ya mwili wake kukutwa Oktoba 4, 2026, majira ya saa 3:20 asubuhi, ukiwa na majeraha ya kukatwa katika kiganja cha mkono wa kulia na kitu chenye ncha kali. Kwa mujibu wa taarifa hiyo, watuhumiwa hao ni miongoni mwa watu zaidi ya 20 waliokamatwa na Jeshi la Polisi kuanzia Septemba 23 hadi Oktoba 21, 2026, kwa tuhuma mbalimbali za uhalifu, ikiwemo mauaji, wizi na makosa mengine ya jinai. Kamanda Mwampaghale amesema upelelezi wa tukio hilo unaendelea, na mara utakapokamilika, watuhumiwa watafikishwa mahakamani kwa hatua zaidi za kisheria. Aidha, Jeshi la Polisi limeendelea kutoa wito kwa wananchi kuzingatia sheria na kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama katika kudumisha amani na utulivu nchini.
Rashid battashy
Region: TZ
Wednesday 21 October 2026 11:55:14 GMT
Music
Download
Comments
official ochu boy :
kumekuchaa xx
2026-10-21 12:47:52
2
RUHAYNA VIJORA PAMBEE :
alhamdulillah
2026-10-21 13:28:34
1
Narmin Niroo :
sasa huku hbr mara mayangazo
2026-10-21 12:55:28
0
Ahmed Aleyy :
Watu 9 mnawashuku tu fanyeni upelelez tena
2026-10-21 13:17:01
0
mudy :
polisiii mung awape nguv tuwajuweee awooo dua kila mda tunasomaa
2026-10-21 13:16:24
0
zuwena608 :
Allah
2026-10-21 13:01:18
1
Suosul :
mwenyezi mungu awape ufahamu mzuri hao wapelelezi wasifanye makosa kumpa kesi asie kuwa na kesi Amin yarab 🙏
2026-10-21 13:29:51
3
abuu fawzaan :
hap kuna mambo haya
2026-10-21 13:31:12
0
WhydahKids🇪🇦🏴💎 :
Hamna kitu wanashuku tu
2026-10-21 13:09:16
0
user9707923226129 :
pambaneni polisi tunawaamini mpaka kieleweke
2026-10-21 13:14:23
0
Mkatalunyatz :
Mwanzo mzuri
2026-10-21 13:25:46
0
Haza Albloushi :
2026-10-21 13:03:53
0
it's dimzy :
kazi nzurii
2026-10-21 12:54:13
0
🥀🤟sailensi kilah 👏💖💖 :
subhanaaallah
2026-10-21 12:53:58
0
nawwar sultwaan :
mhhh haya tutashuhudia mengi acha tuone
2026-10-21 13:01:19
0
Husna Mazrui :
kuiyo ukiuwa hukumu uliwe sio ufungwe haki ifanyike iwe funzo Kwa wengine sio waende gerezaninkula sembe
2026-10-21 13:20:13
1
Abdulhamil :
🥰🥰🥰
2026-10-21 12:59:06
0
To see more videos from user @rashidbattashy, please go to the Tikwm
homepage.