@knews24.media: WANAWAKE WAWILI WAKUTWA WAMEFARIKI DUNIA, WAMEFICHWA UVUNGUNI MWA KITANDA MBEYA Wanawake wawili wamekutwa wamefariki dunia na miili yao kufichwa uvunguni mwa kitanda katika chumba kimoja cha nyumba ya kulala wageni iitwayo Igogwe, iliyopo Mtaa wa Makunguru, Kata ya Ruanda, Tarafa ya Iyunga, jijini Mbeya, huku mmoja wa marehemu akitambulika kwa jina la Annastazia Mwakipesile, mwenye umri wa miaka 32. Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limethibitisha kutokea kwa tukio hilo, likieleza kuwa taarifa za kupatikana kwa miili hiyo zilitolewa Oktoba 16, 2026, majira ya saa 11:45 alfajiri, na Nice Kabuje, mhudumu wa nyumba hiyo ya kulala wageni. Mwili wa pili bado haujatambuliwa na umehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya. Katika kuwasaka waliohusika na mauaji hayo, Jeshi la Polisi lilifanikiwa kumkamata Benson Steven, maarufu kwa jina la Mkembo, fundi sofa na mkazi wa Iwambi jijini Mbeya, Oktoba 21, 2026, majira ya saa 9 alasiri, eneo la Iyela jijini humo. Kwa mujibu wa uchunguzi wa awali wa Jeshi la Polisi, chanzo cha mauaji hayo kinadaiwa kuwa ni imani za kishirikina zilizolenga kupata utajiri, huku mtuhumiwa akieleza kuwa kabla ya kutekeleza kitendo hicho alikwenda kwa mganga wa jadi kwa ajili ya kupata masharti ya utajiri. Jeshi hilo limeeleza kuwa mtuhumiwa alikubali kwa hiari yake kuwaongoza askari kwenda nyumbani kwa mganga huyo. Hata hivyo, wakiwa njiani, mtuhumiwa aliruka kutoka kwenye gari na kuanza kukimbia, hali iliyosababisha askari kufyatua risasi tatu hewani kwa lengo la kumtahadharisha na kumtaka asimame. Kwa mujibu wa taarifa hiyo, baada ya mtuhumiwa kuendelea kukimbia, askari alifyatua risasi iliyompata katika paja la mguu wa kushoto. Mtuhumiwa alikimbizwa katika Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya kwa ajili ya matibabu, lakini alifariki dunia akiwa anaendelea kupatiwa matibabu. Aidha, kumbukumbu za Jeshi la Polisi zinaonesha kuwa Benson Steven aliwahi kukamatwa jijini Dar es Salaam na kushtakiwa kwa kosa la kuvunja nyumba usiku na kuiba, ambapo alitiwa hatiani na kuhukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela. Baada ya kumaliza kifungo hicho, alihamia jijini Mbeya. Pia, taarifa zinaonesha kuwa Desemba 29, 2025, mtuhumiwa alikamatwa eneo la Iwamb. #SautiyajamiiChanzochaUkweli
knews24 media
Region: TZ
Thursday 22 October 2026 17:42:07 GMT
Music
Download
Comments
cutefelly :
msimamiz wa RPC anamacho mazur jmn☺️
2026-10-22 21:15:39
17
Mommy🤍🦋mom🛍️ :
Me at mpenzi wangu namuogop jamanii😳🥺
2026-10-23 06:02:58
6
Jojo sanga 🥰 :
fanyeni mpango police waongezewe mishahala
2026-10-23 05:22:03
9
Madam---Tau :
askar wetu Mungu awalinde
2026-10-23 07:24:31
2
It’s Isabbela 🦋🦕 :
samahani afande naomba namb za uyo msimamizi
2026-10-23 07:44:53
1
Priget Mmari :
Hii habar niliisubir sana
2026-10-22 19:17:27
4
rehemababy :
ingekua vizuli zaidi huyo mganga angekamatwa mana watu wengiwanataka utajili atakua anawapa njia hiyohiyo yakuua watu😭😭
2026-10-23 01:17:05
3
Mrs me😊🦋🔐❤️ :
Ila utajiriii🙌🏼🙌🏼🙌🏼🙌🏼
2026-10-23 01:02:51
2
HARMONAIZE MBEYA🍄 :
mungu atulinde kwakweli ase 🤝🤝🤝
2026-10-22 21:15:15
2
BAD GAL MBEYA NZIMA😂1-5 :
Ndugu zangu hotelia receptionist nawakumbusha tu kuwasajili wateja wetu🥹🙌🏻kwenye kitabu
2026-10-22 21:30:25
3
A.H.T💎💎💎👑 :
mh dada zetu mungu awasaidie na kaz zao za baa
2026-10-23 05:10:08
0
marthasibale1 :
ANNA NDUGU YANGU NTAKUMISI KIPENZI.
2026-10-23 05:48:33
0
Madonina🦄🦄🍇🍇 :
mnisaidiye namba za mganga plz
2026-10-23 09:43:50
0
Ezra Tandale :
mungu mwema
2026-10-23 06:38:36
0
chimama :
polen wafiwa
2026-10-23 05:35:09
0
Aive Abely :
pesa hizii
2026-10-22 20:03:19
0
Madam---Tau :
mbeya yangu😭
2026-10-23 07:22:47
0
Mrs me😊🦋🔐❤️ :
Doh 💔jmn jmn
2026-10-23 00:57:20
0
Rosemary Philipo :
Mhuuu
2026-10-22 20:45:01
0
Frola Mwaitege :
duuuu
2026-10-22 20:46:24
0
marrymangee :
jamani jamani
2026-10-23 10:56:24
0
silentenergy04 :
mwee
2026-10-23 00:36:39
0
Nanabeautybeautify :
du
2026-10-22 21:07:00
0
user3101519945kipany :
tufanye kazi jaman
2026-10-22 21:19:00
0
Reymlawa :
hatar san mungu tusaidie
2026-10-22 19:41:31
0
To see more videos from user @knews24.media, please go to the Tikwm
homepage.