@realsawako555:

สตัง
สตัง
Open In TikTok:
Region:
Friday 23 October 2026 05:47:21 GMT
1399
88
0
4

Music

Download

Comments

There are no more comments for this video.
To see more videos from user @realsawako555, please go to the Tikwm homepage.

Other Videos

Miaka 40-55+ ni kipindi kigumu ambacho hakuna mtu anawaandaa wanawake vizuri. Ni kipindi cha mabadiliko ya homoni - perimenopause na menopause. Hapa ndipo mwanamke anahitaji kujijali zaidi kuliko alipokuwa na miaka 25. Zingatia hivi vitatu, sio kwa urembo tu, ni kwa uhai wako: 1. MIFUPA YAKO - Isiporudi nyuma, utajutia miaka 60 Baada ya miaka 40, homoni ya estrogen inayolinda mifupa inaanza kushuka. Mifupa inaanza kuwa nyepesi - Osteoporosis. Hutaisikia leo, utaisikia ukianguka kidogo tu nyumbani unavunjika kiuno. Zingatia: - Calcium na Vitamin D kila siku: Maziwa, dagaa, mchicha, mayai, na jua la asubuhi dakika 15. Sio dawa tu. - Mazoezi ya kubeba uzito wako: Kutembea haraka, kupanda ngazi, kubeba ndoo ndogo, sio kukaa tu. Kukaa ndio adui wa mifupa. - Punguza soda na chumvi nyingi: Zinaondoa calcium kwenye mifupa. 2. MOYO NA MISHIPA YA DAMU - Hatari inaanza hapa Kabla ya miaka 40, estrogen ilikuwa inakulinda na presha na moyo. Ikishuka, ulinzi unaisha. Wanawake wengi wanapata presha, kisukari na stroke kuanzia miaka 45-55. Zingatia: - Pima presha na sukari kila baada ya miezi 3, hata kama hujisikii mgonjwa. Magonjwa haya hayana dalili za mapema. - Uzito eneo la tumbo: Kitambi baada ya miaka 40 sio urembo, ni hatari ya moyo. Punguza wanga mweupe mwingi - mkate mweupe, soda, pombe. Ongeza mboga na nafaka kamili. - Usingizi:Kukosa usingizi kwa sababu ya joto usiku (hot flashes) kunaongeza presha. Tafuta namna ya kulala masaa 7. 3. AFYA YAKO YA AKILI na huko - Ndio watu hawaongei kabisa Hapa kuna ukweli mchungu: - Uke unakuwa mkavu kwa sababu estrogen imeshuka, tendo linakuwa chungu, hamu inapungua. Wanawake wengi wananyamaza na kuteseka, ndoa zinaharibika kimya kimya. - Hasira za ghafla, kulia bila sababu, kusahau vitu, kukosa hamu ya watu - sio uchawi, ni homoni zinabadilika. - Hii sio aibu. Zingatia: - Usinyamaze: Ongea na mwenza wako,
Miaka 40-55+ ni kipindi kigumu ambacho hakuna mtu anawaandaa wanawake vizuri. Ni kipindi cha mabadiliko ya homoni - perimenopause na menopause. Hapa ndipo mwanamke anahitaji kujijali zaidi kuliko alipokuwa na miaka 25. Zingatia hivi vitatu, sio kwa urembo tu, ni kwa uhai wako: 1. MIFUPA YAKO - Isiporudi nyuma, utajutia miaka 60 Baada ya miaka 40, homoni ya estrogen inayolinda mifupa inaanza kushuka. Mifupa inaanza kuwa nyepesi - Osteoporosis. Hutaisikia leo, utaisikia ukianguka kidogo tu nyumbani unavunjika kiuno. Zingatia: - Calcium na Vitamin D kila siku: Maziwa, dagaa, mchicha, mayai, na jua la asubuhi dakika 15. Sio dawa tu. - Mazoezi ya kubeba uzito wako: Kutembea haraka, kupanda ngazi, kubeba ndoo ndogo, sio kukaa tu. Kukaa ndio adui wa mifupa. - Punguza soda na chumvi nyingi: Zinaondoa calcium kwenye mifupa. 2. MOYO NA MISHIPA YA DAMU - Hatari inaanza hapa Kabla ya miaka 40, estrogen ilikuwa inakulinda na presha na moyo. Ikishuka, ulinzi unaisha. Wanawake wengi wanapata presha, kisukari na stroke kuanzia miaka 45-55. Zingatia: - Pima presha na sukari kila baada ya miezi 3, hata kama hujisikii mgonjwa. Magonjwa haya hayana dalili za mapema. - Uzito eneo la tumbo: Kitambi baada ya miaka 40 sio urembo, ni hatari ya moyo. Punguza wanga mweupe mwingi - mkate mweupe, soda, pombe. Ongeza mboga na nafaka kamili. - Usingizi:Kukosa usingizi kwa sababu ya joto usiku (hot flashes) kunaongeza presha. Tafuta namna ya kulala masaa 7. 3. AFYA YAKO YA AKILI na huko - Ndio watu hawaongei kabisa Hapa kuna ukweli mchungu: - Uke unakuwa mkavu kwa sababu estrogen imeshuka, tendo linakuwa chungu, hamu inapungua. Wanawake wengi wananyamaza na kuteseka, ndoa zinaharibika kimya kimya. - Hasira za ghafla, kulia bila sababu, kusahau vitu, kukosa hamu ya watu - sio uchawi, ni homoni zinabadilika. - Hii sio aibu. Zingatia: - Usinyamaze: Ongea na mwenza wako, "mwili wangu unabadilika, nahitaji uvumilivu". Kunyamaza ndio chanzo cha misuguano. - Lubricant na maji mengi: Ukavu ni wa kawaida, kuna gel salama za kusaidia, Niulize nikusaidie, usivumilie maumivu. - Tafuta marafiki wa rika lako: Kuzungumza na wanawake wenzako wa miaka 45-55 wanaopitia hivyo hivyo inakupunguzia msongo kuliko kukaa peke yako ukidhani wewe tu ndiye unayeteseka. Bonus ya 4 ambayo madaktari wengi wanasahau kusema: Pima saratani. Miaka 40+ ndio wakati wa: - Kupima saratani ya matiti mwenyewe kila mwezi na hospitali kila mwaka - Kupima saratani ya mlango wa kizazi (VIA au Pap smear) Hizi ni vipimo vinavyookoa maisha kama ukichelewa ni gharama kubwa. Hii ni elimu ya jumla tu. Kila mwanamke anapitia mabadiliko tofauti. Kama una jasho jingi usiku, hedhi inaruka-ruka, au presha inapanda, tafadhali usivumilie Kwasasa kipi kinakusumbua zaidi Andika kwenye comments nitakusaidia namna ya kukitatua na kuenjoy maisha yako follow for more women health tips #womenhealth #afyayamwili #premenopose #menopose #ElimuYaAfya

About