@hubofwisdom.inc: Katika ajira, mara nyingi unatumia muda na nguvu zako kutengeneza pesa. Lakini katika biashara, unajenga mfumo unaoweza kutengeneza pesa hata bila wewe kufanya kila kitu mwenyewe. Hapa ndipo dhana ya LEVERAGE inapoingia Leverage ni uwezo wa kutumia rasilimali kama watu, fedha, teknolojia na mifumo ili kuzalisha matokeo makubwa kuliko unavyoweza kwa nguvu zako pekee. Mfanyakazi anatumia muda wake kuzalisha kipato, lakini mfanyabiashara mwenye mfumo anatumia leverage kuongeza uzalishaji na kukuza kipato. Ndiyo maana unaweza kufanya kazi kwa bidii sana, lakini ukazidiwa kipato na mtu ambaye amejenga mfumo unaofanya kazi kupitia watu wengine na teknolojia. Hata hivyo, si kila mwenye biashara ana leverage. Kama biashara yako haiwezi kuendelea bila wewe kuwepo, huenda umejitengenezea ajira nyingine tu! Ajira si mbaya, na biashara si tiketi ya moja kwa moja ya utajiri. Lakini biashara yenye mfumo imara ina uwezo mkubwa zaidi wa kupanuka bila kutegemea muda wa mmiliki pekee. Lengo si kufanya kazi kwa bidii maisha yako yote, bali kujenga kitu ambacho matokeo yake hayategemei nguvu zako pekee. SWALI: Je, kwa sasa unafanya kazi kutengeneza pesa, au unajenga mfumo wa kukutengenezea pesa? Tukamate kwenye YouTube @hubofwisdom.inc tushishiane akili za mtaa #Thewisetz #Leverage #Biashara #Ujasiriamali #FinancialFreedom

hubofwisdom.inc
hubofwisdom.inc
Open In TikTok:
Region: TZ
Friday 23 October 2026 06:26:31 GMT
25710
1372
16
108

Music

Download

Comments

saydeahmed177
sayde ahmed :
leo haujaonhea ukweli.sikubaliani na wew
2026-10-23 09:15:40
1
allymohamedshehe
Ally mohamed Shehe :
utafanyaje biashara bila kusmamia mwenyeo na kitu chochote lazima uwepo usimamizi wako doesn't make sense🤣
2026-10-23 08:43:31
0
gadafijumazaburi
ZABURI :
kwaiyo wakifanya wengine itakuwa hausimamii?😂
2026-10-23 09:11:08
0
bonnie38239
🇹🇿BONNIE 🔥💯 :
hamjamwelewa jaman anamaanisha QNET na network marketing zingine
2026-10-23 12:55:39
0
jumo.harder
jumo harder :
nimemwelewa vema kabisa mwangalieni bakhresabutamkuta ofisi ipi yupo nyumbani biashara zinaenda.unatakiwa uwe mtu wa ubunifu ajiri walioendabshule wrka system
2026-10-23 10:52:34
0
mariam.kamagishom
Mariam KamagiShoma's Family :
🥰🥰🥰
2026-10-23 06:43:21
0
user84670714988
Elias Zacharia Elias :
wazi
2026-10-23 08:09:06
0
kirschsten
KIRSCHSTEIN :
kwel kabisa, 💯
2026-10-23 10:17:32
0
kelvin_mveti
kelvin_Mveti :
Kabisa yan😅
2026-10-23 08:25:42
0
mwandu533
Madonna :
😂😂😂
2026-10-23 09:09:56
0
sdt1104
SDT :
👏
2026-10-23 09:33:35
0
profesa.jerryfive
Profesa Jerryfive Tz :
ujasiriamali = kitendo cha kubuni bidhaa au huduma kuleta kwenye jamii & Biashara = kuuza na Kununua haijalishi uwepo wako kazi = nishughuli yoyote inafanyika au kumilika kwa kuzingatia uwepo wako tu mara zote kwahiyo ilijiite wewe ni Mfanyabishara = nipale tu mipango ya shughuli zako zinapo fanyika na kusimamiwa kwa Kutumia Mifumo Maalumu bila Kuhutaji Uwepo wako lakini Ukiwepo Tayari unakuwa Umejiajiri kuajiriwa sio Mfanyabiashara kazi yako =hairithiki Biashara =hurithika # Eng Kabenda # Mwalimu Cosmas
2026-10-23 13:32:26
0
To see more videos from user @hubofwisdom.inc, please go to the Tikwm homepage.

Other Videos


About