@jambotv_: VIDEO: Mkuu wa Wilaya ya Babati, Hashimu Mgandilwa, amewataka wenyeviti wa serikali za mitaa na vijiji kuzingatia majukumu yao ya uongozi na kujishughulisha na shughuli nyingine za uzalishaji mali, badala ya kutumia muda mwingi kukaa ofisini bila sababu za msingi. Mgandilwa ametoa kauli hiyo jana Oktoba 22, 2026 katika kikao na wenyeviti wa mitaa na vijiji, watendaji wa mitaa na vijiji pamoja na watendaji wa kata, kilicholenga kuwakumbusha viongozi hao majukumu yao na kuweka uelewa wa pamoja kuhusu utekelezaji wake ili kuepusha mkanganyiko kwa wananchi. Amesema nafasi za uenyekiti wa serikali za mitaa na vijiji hazimaanishi kuwa viongozi hao wanapaswa kukaa ofisini kuanzia wakati wa kufunguliwa hadi kufungwa, akisisitiza kuwa walitakiwa kuwa na shughuli nyingine za kujipatia kipato walipoomba nafasi hizo. “Wenyeviti wa vijiji, wenyeviti wa serikali za mitaa, nafikiri ni jambo ambalo tunalifahamu wakati wa uchukuaji wa fomu ambazo zimetupa nafasi hizi ambazo tunazitumikia. Fomu ile ilitutaka tuwe na shughuli nyingine za kujipatia kipato, sasa wapo wenyeviti ambao wanataka ofisi inapofunguliwa awepo ofisini mpaka inafungwa, si kazi yenu,” amesema DC Mgandilwa. Amesisitiza umuhimu wa viongozi hao kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia mahitaji ya wananchi, huku wakiendelea na shughuli nyingine za uzalishaji mali zinazowawezesha kujipatia kipato.

Jambo TV
Jambo TV
Open In TikTok:
Region: TZ
Friday 23 October 2026 07:06:21 GMT
28047
397
18
104

Music

Download

Comments

dany_jr2026
dany :
Wakianza kubwa na biashara,mnakuja kusema hawafanyi kazi wanakula mshahara wa bure
2026-10-23 10:04:40
1
lindekalindeka377
lindekalindeka377 :
ikitokea zarula akiitwa mutamlipa Tanzania Sheria na kanuni hazipo sawa
2026-10-24 09:27:59
0
greatsizala
The gbs :
Facts
2026-10-23 07:53:55
1
jadan_athuman
user5945129904850 :
kuna.shd xn kw wenyevt
2026-10-23 18:06:59
0
seyphujuma
[email protected] :
sio kweli
2026-10-24 05:12:02
0
mathiasluhwavi1
nyoka :
amemsaidia nini kwani watendaji hawachukui lushwa tena hawa wenyeviti ndo huwa wanajitahid kuwazuia
2026-10-23 19:43:26
0
mathayo.laizer21
Mathayo Laizer :
mkuu takwa metuasdia kabisa mkuu
2026-10-23 18:12:50
0
simonmnakey
sai mnakey👋 :
ccm ni ugonjwa
2026-10-23 19:19:40
0
mr.tarimo1
Mr.tarimo :
😂😂😂 hii Tanzania bhna
2026-10-23 11:36:58
0
kasimuhalili
Kasimu Halili :
ila ni watu muhimu sana Hawa tena sana
2026-10-23 20:05:46
0
josephngoma3762
mdundo :
wakiwa busy mnaanza kuwasema tena
2026-10-23 19:34:29
0
nuru.magohe6
Nuru Magohe :
tena uko sahihi kabisa mkuu. twanga kazi.
2026-10-23 18:31:01
0
daniel.mbwambo2
Daniel Mbwambo :
wanaolipwa wachukue majukumu ya serikali sioni haja ya mw/kiti
2026-10-23 17:07:52
0
nuru.magohe6
Nuru Magohe :
najiuliza hivi hii ngazi ya mwenyekiti kwa nini isifutwe tu? kuliko kukaa na kushambuliana kila kukicha. Wabaki watendaji tu kelele ziishe. Hawajajiweka hapo wala mihuli hawajaichonga wao. I
2026-10-23 18:22:56
0
ntemi.4g.general
NTEMI 4G GENERAL SUPPLIER :
f
2026-10-23 09:05:25
0
kasimuhalili
Kasimu Halili :
futeni hicho cheo
2026-10-23 20:06:42
0
To see more videos from user @jambotv_, please go to the Tikwm homepage.

Other Videos


About