@bongo_media: 2026-10-24 Actress na content creator, Anty Habiba maarufu kama Queen Kukiii, ametoa ujumbe mzito kwa wanawake wanaojilinganisha na wanawake wanaopata fedha kupitia biashara au shughuli mbalimbali za mitandaoni, akiwataka kuacha kushindana na wengine na badala yake kuthamini mahusiano yao. Queen Kukiii amesema kuwa si kila mwanaume anayeshindwa kutoa fedha nyingi kwa mwenza wake hana uwezo wa kumhudumia, bali wakati mwingine wanawake hujiwekea matarajio makubwa kwa kujilinganisha na wale wanaopata fedha kutoka kwa wanaume wengi. Akieleza msimamo wake, Queen Kukiii amesema kuwa yeye anathamini namna mume wake anavyomhudumia na kumpa mahitaji yake, huku akisisitiza kuwa mwanamke mwenye mwenza mmoja hapaswi kujilinganisha na mtu anayepata fedha kutoka kwa watu wengi. “Sio kwamba mwanaume wako hajui kuhudumia, tatizo unataka kushindana na wanaojiuza. Unataka kushindana na maslahi ya mtandaoni,” amesema Queen Kukiii. Aidha, amewataka wanawake kutambua kuwa kujilinganisha na maisha ya watu wengine kunaweza kuleta migogoro katika mahusiano yao, akisisitiza umuhimu wa kuridhika na kuthamini kile ambacho wenza wao wanaweza kuwapatia. Kauli hiyo imeibua mjadala kuhusu mahusiano, fedha na matarajio ya wanawake kwa wanaume wao katika kipindi hiki ambacho mitandao ya kijamii imekuwa sehemu ya maisha ya kila siku. Je, unakubaliana na @queen_kukiii kwamba wanawake wanapaswa kuacha kujilinganisha na wengine katika mahusiano? Toa maoni yako.
BONGO MEDIA
Region: TZ
Saturday 24 October 2026 13:06:46 GMT
Music
Download
Comments
nadya_🌹🌹 :
[Laugh approved][Laugh approved][Laugh approved][Laugh approved][Laugh approved]wallah
2026-10-24 18:55:45
0
Chibebe🦋❤️ :
Wapambanaji 😂
2026-10-24 18:54:13
1
Michael John :
Yes wambie
2026-10-24 18:36:47
0
𝐁♡ :
Asante😂🤲
2026-10-24 18:50:51
0
HAMZA THE DON :
kuongea fact
2026-10-24 16:17:27
11
master RB :
saf kabisa fact ya kwenda kabisa
2026-10-24 17:02:40
6
🚭Łïķø jüñïôř🌿 :
Asante sana kwa kuwakumbusha [Tears of joy][Tears of joy][Tears of joy]
2026-10-24 17:07:44
5
champion kid :
aiiiiiiiiiihhhhh wakumbushe dada
2026-10-24 17:20:42
2
geza ulole :
mbona siwaoni hapa😂😂
2026-10-24 18:53:40
0
kindamba jr :
yamenikuta mieeee
2026-10-24 15:08:10
4
SWALEHE :
mke wangu muone uyu
2026-10-24 15:03:58
5
Judy Emmanuel 🥰 :
Kabisa da mzuri
2026-10-24 15:00:55
2
Vipperbillgate’s🚀🚀🗼🏖 :
point iyoo
2026-10-24 15:34:27
2
Edoo John :
Yambie ukweli
2026-10-24 16:40:05
1
Girl friend💃💋❤️😘 :
Ni kwer mpnz
2026-10-24 18:38:33
0
KiTAO JR🐐🐐🐐 :
NAMBA yako ya M-PESA please
2026-10-24 16:59:14
0
salima :
2026-10-24 14:43:55
2
MR-SUCCE$$ :
Sijui nikaweke status au kuna mtu nita mkwaza 🤣🤣🤣
2026-10-24 18:01:25
0
mzaramo :
mungu akuweke dada
2026-10-24 14:32:50
1
Petro Julius :
bola umeongea
2026-10-24 14:08:58
0
smoker :
kwisha
2026-10-24 16:03:25
0
kilumbujr :
Kabisa
2026-10-24 16:47:39
0
K.B+255tz :
bora muambiane wenyewe
2026-10-24 14:12:15
0
@ KING 👑ZEDE✅ :
hapo kuna mambo haya✌️
2026-10-24 15:04:42
0
natu_vincere :
😂😂😂 unaongea ukwel sana😁😁😁
2026-10-24 13:52:07
0
To see more videos from user @bongo_media, please go to the Tikwm
homepage.