@jicholaupendo: #Repost @polisi.tanzania WALIA NA BODABODA, WAOMBA UJENZI WA KITUO CHA POLISI UKAMILIKE Wakazi wa Kata ya Luchelele wilayani Nyamagana mkoani Mwanza wameiomba Serikali na Jeshi la Polisi kuwachukulia hatua madereva pikipiki (Bodaboda) wanaobadilisha pikipiki zao kwa kuziongezea milio mikubwa jambo linalowashtua huku wakihimiza ukamilishwaji wa kituo cha polisi kilichojengwa kwa muda mrefu bila kukamilika. Kilio hicho kimetolewa Oktoba 24, 2026, wakati wa mkutano wa Kampeni ya ‘Ongea na Kamanda wa Polisi’, uliofanyika katika kata hiyo kwa lengo la kusikiliza kero za wananchi na kutafuta suluhisho la changamoto za kiusalama. Akichangia katika mkutano huo, Mkazi wa Kisoko, Josephina Anthony, alisema milio ya pikipiki hizo imekuwa ikileta hofu kwa wananchi, hasa nyakati za usiku, ambapo baadhi yao hupata mshtuko na kudhani kuwa kuna milipuko au hatari nyingine. Alimwomba Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, DCP Wilbrod Mutafungwa, kuchukua hatua dhidi ya waendesha bodaboda wanaosababisha kero hiyo ili wananchi waweze kuishi kwa amani na utulivu. Naye Mkazi wa kata hiyo, Zabroni Juma alieleza kusikitishwa na kuchelewa kukamilika kwa ujenzi wa kituo cha polisi cha Luchelele, akiiomba Serikali na wadau wa maendeleo kuweka juhudi za makusudi kuhakikisha kituo hicho kinakamilika ili kusogeza huduma za kipolisi karibu na wananchi. Akijibu hoja hizo, DCP Mutafungwa alisema Jeshi la Polisi kupitia askari wa Usalama Barabarani litaendelea na operesheni dhidi ya waendesha pikipiki wanaofanyia mabadiliko vyombo vyao vya moto na kuvifanya kutoa sauti zisizolingana na zile zilizotengenezwa navyo. Alieleza kuwa mabadiliko hayo ni kosa na yanaweza kusababisha hofu kwa wananchi, huku milio hiyo wakati mwingine ikifanya iwe vigumu kutofautisha sauti za pikipiki na milipuko inayoweza kusababisha madhara. Alisisitiza kuwa pamoja na operesheni na hatua za kisheria dhidi ya wanaokiuka taratibu, elimu kwa waendesha pikipiki ni muhimu ili kuwasaidia kubadili tabia na kuzingatia sheria za usalama barabarani. Kuhusu ujenzi wa kituo cha Polisi cha Luchelele, Kamanda Mutafungwa alieleza umuhimu wa kukamilisha kituo hicho kwa wadau wote ili wananchi waweze kupata huduma za kipolisi kwa urahisi
jicho la upendo
Region: TZ
Sunday 25 October 2026 10:19:41 GMT
Music
Download
Comments
Miry Lyker :
me wananiudhig 🥺
2026-10-26 09:35:54
0
kulu majiwe 🥰 :
Ni yeyeee🤣🤣
2026-10-25 16:36:59
128
clarachriss4 :
ni hoja ya msingi wala sio kucheke😟😟
2026-10-25 16:31:34
154
it's muu💖🦋✨️ :
yaan wanakera sana hasa ukiwa na stress 😂😂
2026-10-25 16:30:23
29
Madam Rachel mliwa :
Asante umewakilisha wanakela sana
2026-10-25 16:08:59
22
recho :
Nikwer mama wanakera ma boda
2026-10-25 13:40:10
101
🎀🎀evar🎀🎀 :
watupunguzie presha kwel
2026-10-25 15:20:23
14
Mwaj..🇹🇿🇶🇦🫶 :
nikweli kabisa jamani
2026-10-25 19:02:49
4
Mama wini Soft drink💞💕💯 :
tena wakisogea karibu na watu
2026-10-26 09:24:57
1
UFANISI ELECTRONICS :
naunga mkono😂😂😂😂
2026-10-25 16:13:53
9
Royder Philimon :
as ante mama kwa kuongelea hill ma a na hat a mie wananikela
2026-10-25 18:41:18
4
blessed-v :
Hata me sipend aise😏
2026-10-25 16:35:18
5
sospeter masula :
Vumilia mama ndo watoto wetu
2026-10-26 05:55:24
1
NANCY PAMBA KALI :
miemwenyewe huwaga nashtukaga sana watatutanuwa miyo
2026-10-25 18:30:42
4
Agness Nkugwe :
Mama niko pamoja na wewe ukweli inakera sana.
2026-10-25 21:10:00
3
careen :
Kwa kweliii 🤣🤣🤣
2026-10-25 17:24:27
2
agines :
nikweli waache kwakweli
2026-10-25 14:03:59
2
user2479434176229 :
Naunga mkono
2026-10-25 22:38:21
1
Afua Lusigi :
Kweli kabisaa Mama
2026-10-25 17:38:34
2
bbhu :
Polic wapo busy kuwasikiliza cccm
2026-10-25 15:25:55
1
ashurakiwanga :
kweli kabisa
2026-10-25 16:33:02
1
Dpascali ✊️ :
Hahahaha😂
2026-10-25 16:26:51
1
rey qeen💞💞💞 :
Kwel hasa arusha
2026-10-25 18:27:20
1
🦋PRETTY 🦋 :
Msije mkafanya challenge jmn🤣🤣🤣
2026-10-25 15:27:43
1
user3888594602226 :
boda wanasemaje
2026-10-25 14:41:18
1
To see more videos from user @jicholaupendo, please go to the Tikwm
homepage.