@bongaplustv: Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Dar es Salaam, Nasra Mohamed, amemtetea Rais Samia Suluhu Hassan dhidi ya madai kwamba hajatekeleza miradi ya maendeleo, akitaja ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) na Bwawa la Kufua Umeme la Julius Nyerere kama mifano ya miradi iliyoendelea na kukamilishwa wakati wa uongozi wake. Akizungumza leo, Oktoba 25, 2026, Nasra amesema mradi wa SGR ulianza wakati Samia akiwa Makamu wa Rais na kwamba reli hiyo imeendelea kujengwa na kutumika katika baadhi ya vipande vyake. Amehoji wanaodai Rais Samia hajafanya miradi yoyote kuangalia hatua iliyofikiwa na mradi huo. Kuhusu Bwawa la Kufua Umeme la Julius Nyerere, Nasra amesema Rais Samia aliendeleza na kukamilisha kazi zilizoachwa na mtangulizi wake, akieleza kuwa hatua hiyo ilikuwa sehemu ya kuendeleza miradi ya kitaifa.
BONGA+ TV
Region: TZ
Sunday 25 October 2026 12:26:37 GMT
Music
Download
Comments
utamu mzuri sana :
nitafutien
2026-10-25 19:09:00
0
pondo cdi 777 :
punguzen siasa atakaz amfanyi nisiasa
2026-10-25 17:07:00
0
ShabyDuduma :
Masha Allah ustadhat
2026-10-25 16:10:27
0
utamu mzuri sana :
mm nimesh mpenda huyu dada kimapnz
2026-10-25 19:08:48
0
youngndike :
👍👍👍👍🙌🙌🙌
2026-10-25 15:53:25
0
To see more videos from user @bongaplustv, please go to the Tikwm
homepage.