@kishkionlinetv: Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, amesema ameliagiza Shirika la Ujasusi la Mossad na Jeshi la Ulinzi la Israel (IDF) kufanya juhudi za kuiondoa madarakani serikali ya Iran, akidai kuwa hatua hiyo ndiyo njia pekee ya kuondoa tishio analodai nchi hiyo inaliletea Israel. Akizungumza katika hafla ya kuhitimu kwa maofisa wa jeshi la Israel Oktoba 25, 2026, Netanyahu alishutumu Iran kwa kujaribu kuendeleza tena mpango wake wa kutengeneza silaha za nyuklia. Alisema Israel inakabiliwa na tishio kubwa la kiusalama na kwamba kuiondoa serikali ya Iran madarakani ni sehemu ya maagizo yake kwa vyombo vya ulinzi na usalama vya nchi hiyo. Netanyahu pia amedai kuwa Israel ina fursa ya kuimarisha amani ya muda mrefu katika Mashariki ya Kati na kupanua uhusiano wake na mataifa ya Kiarabu. Kauli hizo zinatolewa wakati mvutano kati ya Israel na Iran ukiendelea, huku suala la mpango wa nyuklia wa Iran likiwa kitovu cha mzozo huo. Iran, kwa upande wake, imekuwa ikipinga madai kuhusu nia yake ya kutengeneza silaha za nyuklia na kuonya dhidi ya mashambulizi mapya ya kijeshi.
Kishki Online TV
Region: TZ
Monday 26 October 2026 16:07:13 GMT
Music
Download
Comments
Muhandas :
ataanza kuondoka yeye kwanza
2026-10-26 19:56:18
0
young swaah :
uchanguz utafanyw tu hata ufanyeje
2026-10-26 17:43:00
0
mr ndiz@ :
😂😂😂😂😂😂
2026-10-26 17:12:58
0
To see more videos from user @kishkionlinetv, please go to the Tikwm
homepage.