@jambotv_: VIDEO: Mkuu wa Mkoa wa Mara, Brigedia Jenerali Evans Mtambi, amekabidhi kinyago cha fisi kwa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime baada ya halmashauri hiyo kushika nafasi ya mwisho katika tathmini ya usafi wa mazingira mkoani humo. Akizungumza wakati wa kukabidhi kinyago hicho leo katika Ukumbi wa Uwekezaji uliopo Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara, Mtambi amesema zoezi la kutathmini halmashauri na kutoa tuzo kwa zinazofanya vizuri au vibaya litafanyika kila mwezi. Katika tathmini ya hivi karibuni, Halmashauri ya Wilaya ya Tarime imekusanya alama 25 kati ya 100, huku Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti ikiongoza kwa kufanya vizuri katika usafi wa mazingira. Kwa upande wake, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mara, Zabron Masatu, akitaja matokeo ya tathmini hiyo, amesema Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti imeongoza kwa kupata alama 70, ikifuatiwa na Manispaa ya Musoma iliyopata 68 na Halmashauri ya Mji wa Tarime iliyopata 65. Halmashauri ya Wilaya ya Musoma imepata alama 55, Bunda DC 40, Rorya 35, Bunda TC 30, Butiama 28 na Tarime DC imepata alama 25. Kinyago hicho kitakuwa ishara ya kutambua halmashauri zinazofanya vibaya katika usafi wa mazingira, ambapo kitakabidhiwa kwa wakuu wa wilaya, wakurugenzi wa halmashauri na maafisa mazingira wa maeneo husika. Hatua hiyo inalenga kuhamasisha ushindani chanya na kuimarisha kampeni ya usafi wa mazingira katika Mkoa wa Mara.

Jambo TV
Jambo TV
Open In TikTok:
Region: TZ
Monday 26 October 2026 17:42:41 GMT
9673
115
6
15

Music

Download

Comments

georgetobias37
georgetobias37 :
at least
2026-10-27 05:39:00
0
user3114961027344
Erasto, nature lover :
serengeti hongera
2026-10-27 12:09:08
0
neina492
Neina :
big up Serengeti DC
2026-10-26 20:38:21
0
laizerandrea813
ALLY SHANTO MBAG :
hapoo kuna mambw hay ✌️
2026-10-26 18:59:59
0
ramadhanjuma185
Rama mishemishe :
Kumbe haya mambo ya bellow fifty bado tu yapo hadi kwenye real life!!!!
2026-10-26 18:04:16
0
alexander.black.am
Alexander the Great 💪🏿 :
Kinyago kinasaidia nini kuongeza ufaulu
2026-10-27 13:00:40
0
To see more videos from user @jambotv_, please go to the Tikwm homepage.

Other Videos


About