@millardayo_: Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Zainab Katimba amesema Mtoto ana haki ya kurithi mali za Mzazi wake bila kujali kama amezaliwa ndani au nje ya ndoa. Katimba ametoa ufafanuzi huo bungeni Jijini Dodoma wakati akijibu maswali ya Mbunge Tina Andrew Chenge, aliyehoji iwapo Serikali haioni umuhimu wa kufanya marekebisho ya sheria za mirathi ili kuhakikisha Watoto waliozaliwa nje ya ndoa hawabaguliwi katika ugawaji wa mali za Marehemu. Akijibu hoja hiyo, Katimba amesema mali zinazoweza kuingizwa kwenye mirathi ni zile zilizokuwa zikimilikiwa kisheria na Marehemu wakati wa kifo chake, huku akifafanua kuwa mali zilizotolewa kama zawadi wakati wa uhai wa Marehemu haziwezi kurejeshwa kwenye mirathi kwa sababu tayari zilikuwa zimetoka katika umiliki wake. Katimba amesisitiza kuwa Sheria ya Mtoto inatambua haki ya Mtoto kurithi kutoka kwa Mzazi wake, iwe amezaliwa ndani au nje ya ndoa, huku akieleza kuwa Serikali itaendelea kuhakikisha haki za Wanawake, Watoto na Warithi wengine zinalindwa kwa mujibu wa Sheria. #MillardAyoUPDATES

millardayo
millardayo
Open In TikTok:
Region: TZ
Tuesday 27 October 2026 10:22:26 GMT
60956
2319
142
106

Music

Download

Comments

luckydeamy3
LuckyHamcy :
kurithi ipo lakin ni jina la baba na la ukoo ila sio vtu nilivyotafuta na mme wngu
2026-10-27 12:18:50
17
jackline.celestin0
Jackline :
Watoto wa nje wanarithi vya nje
2026-10-27 13:25:07
7
victoriagavana
Vivi :
over my deadbody
2026-10-27 12:46:19
0
irenemchagaa
Irene mchaga :
heeeeeeeee tumekwishaaa
2026-10-27 12:24:06
0
user661011868530
Makaranga’s Daughert :
na kama kwa mfano mume anaenioa alikua ameoa wakaachana kwa divorce na wakagawana kila kitu na huyo mkewe au kila kitu akamuachia mkewe na watoto mm tumepatana tuakaanza kutafuta upya ikitokea Mume wangu anakufa na wale watoto watagawana hizo mali ama vip msaada
2026-10-27 11:41:43
3
allydaddy80
my name is.. :
me nilijua mapema sina changu kwa baba nimepambana nimepata vyangu maana ata jina nimepewa la babu
2026-10-27 10:58:38
16
brandb6460
ROSE BRAND🌹🦋 :
hakunaaa hyoooo
2026-10-27 10:28:27
5
officiallight564
officiallight :
tunashukuruu selikali ya tz tumefikiwa
2026-10-27 11:55:35
4
mapalogamba8
mapalo gamba 🤴 👑 :
first comment
2026-10-27 10:27:13
1
nancydaniel247
Nancy💓 :
mnatufanya tujiwekeze sana sisi wanawake zaidi kwa siri kuliko kutoa jasho lako kwa watoto ambao mume kakutesa nao na mwanamke huyo kamchuna huyo baba na amewekezea watoto wake alafu chakwangu kidogo nilichopambana nacho tugawane tena pamoja🙌tafakarini hilo je watoto wangu wanaishije?
2026-10-27 12:08:12
3
suzy84221
suzy :
mi mwanangu marufuku kulilia vitu vya urithi akatafute vya kwake unarithi vitu hata hujui kavipata wap mim mwanangu marufuku kabsa
2026-10-27 11:50:04
4
prat_nito1
prat_nito1 :
Hapo itachangia ongezeko la watoto wa nje ya ndoa
2026-10-27 14:10:32
1
ummuh428
ummuh❤️😍 :
baba yangu jifiche kuzaa nje siku imefika wajitokeze watu kudai urithi 😂 hawata amini macho Yao Yani hawaambulii chochte hiyo ni Sheria yangu Sasa
2026-10-27 10:44:24
3
user5851116939657
enjo mayemba :
me ajichanganye mtu ataambulia atakacho kitafuta heeeeeeee,
2026-10-27 12:30:15
1
teknol96
🤯teknol$@ :
kwani ikitokea mama kazaa njee kabla hajaolewa na mama ake akaolewa na kupata maali yeye anawekwe wap
2026-10-27 12:02:10
3
yvonnemtono
yvonne🩺 :
Mungu endelea kuniondolea tamaa...cjui hata haki zangu na wala ctaki kujua nipewe uwezo wa kutfta tu vya uzao wa tumbo langu nikifa wasiende kutia huruma kwa baba yao ambae ana mke mwingne 💔dear lord naomba kibali cha umiliki halali 🙏🏽🧎🏽‍♀️
2026-10-27 11:50:26
3
tz777279
Junior Juniorjunior :
yaani hapo hatufanyi maendeleo kwa mwanaume
2026-10-27 11:34:14
1
mr.nova67
Nana Oisso✨💫💦🥳 :
Mwanaumeee awekezeee na Mwanamkeee wakeee walo zaaaa hakikishaaa ukizaaa na mtuu akupeee cha kuridhii Mapemaaa
2026-10-27 12:41:16
1
jesussever
# testimony 🙌 🙏 :
sa kama nimeolewa nishazaa mtoto wangu anarithi🔥
2026-10-27 13:22:27
0
tunuhabibu492
Tunu Habibu :
amechuma na nani izo mali
2026-10-27 11:32:36
0
olivia.joram
Olivia Joram :
kwanini asimtafutie hukohuko walikokutana kwangu wasijaribu kugusa mali zangu
2026-10-27 12:43:17
1
lambada4207
Aim baby Mom omani🇧🇬 :
Mie acha nijenge mwenyewe mambo ya kujenga wote mwisho wa siku watoto wanje awatumii nguvu apana🙌
2026-10-27 13:57:57
1
estherjoseph916
estherjoseph9646 :
jamani wamejuwaje
2026-10-27 11:12:42
0
elialebere
Five star 💫 :
Nchi isiyo na mwenyew inawashinda mnajadili mambo ya family zenye wenyew
2026-10-27 12:21:03
1
josephina.lucas
josephina.lucas :
Kila mtu atafute zake kwekweli
2026-10-27 11:46:02
1
To see more videos from user @millardayo_, please go to the Tikwm homepage.

Other Videos


About