@muhimbili_mloganzila: Changamoto ya kuharibika kwa mimba katika miezi mitatu ya mwanzo ya ujauzito huwakumba wanawake wengi. Ni sababu zipi zinazoweza kusababisha mimba kuharibika katika kipindi hiki? Ungana na Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Wanawake na Afya ya Uzazi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila, Dkt. Hillary Kizwi, akifafanua sababu za hali hii na mambo muhimu ya kuyafahamu.