@tonychungne: Vệ sinh máy giặt Fasclean cao cấp#Tonychung #tiktokshop

Tony Chung
Tony Chung
Open In TikTok:
Region: VN
Wednesday 28 October 2026 10:29:00 GMT
377
2
0
1

Music

Download

Comments

There are no more comments for this video.
To see more videos from user @tonychungne, please go to the Tikwm homepage.

Other Videos

ASKOFU MKUU RUWA’ICHI: UPENDO, UTII NA USIKIVU NI MSINGI WA FAMILIA IMARA Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mhasham Jude Thaddeus Ruwa’ichi, O.F.M.Cap., amesisitiza kuwa familia haziwezi kustawi bila upendo wa kweli, utii na usikivu kati ya wanandoa, akionya kuwa tabia ya wanandoa kukwepana ni ishara ya kukosekana kwa misingi hiyo muhimu katika maisha ya familia. Akihubiri katika Misa Takatifu ya kumpongeza kwa Jubilei ya Miaka 50 ya Utawa, iliyoadhimishwa katika Parokia ya Mivumoni, Jimbo Katoliki la Bagamoyo, amesisitiza kuwa upendo wa kweli si maneno matupu, bali ni wajibu unaodai kujitoa, kujituma na kujisadaka kwa ajili ya ustawi wa familia. Akifafanua wajibu wa mume na mke, Askofu Mkuu Ruwa’ichi amesisitiza kuwa mafundisho ya Neno la Mungu kuhusu utii katika ndoa hayapitwi na wakati, akieleza kuwa wito wa mke kumtii mume wake haupaswi kutenganishwa na wajibu wa mume kumpenda mke wake. Amesema mume na mke wote wanawajibika kuishi katika upendo, utii na usikivu, wakijali maslahi ya wenzao na ya watoto wao, huku akisisitiza kuwa kumpenda mwenzi wako kunapaswa kuonekana katika matendo ya kila siku ya kujali na kuwajibika. Katika sehemu yenye msisitizo wa wazi, Askofu Mkuu Ruwa’ichi ameonya kuhusu tabia ya baadhi ya wanandoa kukwepana, akitoa mfano wa mume anayechelewa kurudi nyumbani au kutafuta sababu za kukwepa uwepo wa mke wake kwa hofu ya kukosolewa au kukabiliwa na migogoro. Ameeleza kuwa hali hiyo inapojitokeza, ni muhimu kwa wanandoa kutafakari upya namna wanavyoishi, akibainisha kuwa pale ambapo hakuna utii, upendo, kusikilizana na kujaliana, msingi wa maisha bora ya familia na ushuhuda wa Kikristo huathirika. Akihitimisha ujumbe wake, amewahimiza wanandoa na familia kwa ujumla kurejesha thamani ya upendo, utii na usikivu katika maisha yao ya kila siku, akisisitiza kuwa familia zinazojengwa katika misingi hiyo zina nafasi ya kustawi na kuwa ushuhuda wa maisha ya Kikristo katika jamii. Imeandikwa na Izahaki B Mwacha. Video Source:MuPhilip Media #KanisaKatoliki #Tanzania #BaloziwaAmani #breezonlinetv #woisooriginalproducts #mkombozicommercialbank #news

About