@breezt4: PADRE JONATHAN MKWIZU AONYA DHIDI YA MATUMIZI MABAYA YA MADARAKA, ASEMA WENYE NGUVU WAMEWAUMIZA WENGI Katibu wa Askofu wa Jimbo Katoliki la Same, Padre Jonathan Mkwizu, ametoa onyo kali dhidi ya matumizi mabaya ya madaraka, akisema baadhi ya watu wenye vyeo na nguvu wamekuwa chanzo cha mateso kwa wengine, wakiwemo wajane na watoto yatima waliopoteza wapendwa wao kutokana na maamuzi ya watu wenye mamlaka. Padre Mkwizu ameyasema hayo wakati wa homilia katika Misa Takatifu ya Dominika ya 30 ya Mwaka A wa Kanisa, iliyoadhimishwa katika Kanisa Kuu la Jimbo Katoliki la Same, akisisitiza kuwa cheo, ulinzi na nguvu alizonazo mtu havimpi haki ya kuwatesa, kuwateka au kutoa amri za kuangamiza maisha ya wengine. Akifafanua ujumbe wa masomo ya siku hiyo, Padre Mkwizu amesema kuna watu wanaotumia mamlaka yao kufanya chochote wanachotaka kwa sababu wana nguvu na ulinzi, huku wakisahau kuwa matendo yao yanaweza kuwa sababu ya watu wengine kulia, kupoteza wenza wao na hata kuishi bila wazazi. “Ni watu wangapi leo wanalia? Pengine ni wajane kwa ukweli wajane kabisa, kwa sababu wewe umekuwa sababu ya ujane wao. Ni wangapi ambao leo pengine wamepoteza wazazi wao kwa sababu ya amri yako wewe mwenye nguvu?” amehoji Padre Mkwizu. Amesema Neno la Mungu katika Kitabu cha Kutoka linatoa onyo kali kwa wale wanaowatesa wageni, wajane na watoto yatima, likisisitiza kuwa Mungu husikia kilio chao na hasira yake huwaka dhidi ya wanaowadhulumu. Padre Mkwizu amesisitiza kuwa onyo hilo halikuhusu Waisraeli pekee, bali linawahusu pia watu wa kizazi cha sasa, akiwataka kujichunguza na kuacha kutumia vyeo, mafanikio na nguvu zao kuwaumiza wengine. Amesema kila mtu anapaswa kujitambua kuwa anamtegemea Mungu, hata anapokuwa na mafanikio, cheo au uwezo mkubwa, kwa sababu kuna wakati katika maisha kila mmoja amewahi kuwa mhitaji na kutegemea msaada wa wengine. Aidha, amewataka watu waliofanikiwa kutosahau walikotoka, akitumia mfano wa Misri kuonyesha hali ya mateso ambayo mtu anaweza kuwa amepitia kabla ya kupata uhuru na maisha bora. “Usisahau Misri yako ukamrudisha mwenzako katika Misri ile ambayo yeye ameipita. Misri ya mtu inaweza ikawa ni mateso makubwa. Usiwe wa kwanza kumpeleka mwenzako Misri baada ya kutoka Misri,” amesisitiza. Ameeleza kuwa Misri ya mtu inaweza kuwa hali ya kukosa mtu wa kumtegemea, kama vile mume kwa mjane au wazazi kwa mtoto yatima, hivyo kuwataka wenye uwezo kutowarudisha wengine katika mateso waliyokwisha kuyapitia. Katika hatua nyingine, Padre Mkwizu ametoa wito wa kutubu na kuomba msamaha kwa Mungu kwa makosa yaliyofanywa kupitia mamlaka, vyeo na nguvu walizo nazo watu, hasa pale ambapo uwezo huo umetumika kuwaumiza wengine. Imeandikwa na Izahaki Mwacha Video Source: Radio Maria Tanzania #KanisaKatoliki #Tanzania #BaloziwaAmani #breezonlinetv #woisooriginalproducts #mkombozicommercialbank #news
Breez Online Tv
Region: TZ
Wednesday 28 October 2026 13:13:57 GMT
Music
Download
Comments
Omona Otata :
Ubarikiwe baba, so painful 😭😭😭
2026-10-29 05:02:19
1
muhhamed :
mfumo kristo umehamaki
2026-10-28 17:11:45
3
Felix Kisaka :
AMEN 👏 TUMSHUKURU Mungu daima Aendelee KUTUBARIKI WATANZANIA Tudumishe AMANI UMOJA na Ushirikiano KITAIFA na KIMATAIFA Tuendelee KUIJENGA NCHI YETU Hatua kwa Hatua ili maadui wa ndani na nje WASHINDWE KABISA Tena WAFIKIE TOBA Wale Wanaopika na kuhamasisha machafuko CHUKI na Vurugu
2026-10-28 15:15:55
3
Asimwe deus :
umeongea kwa hisia baba barikiwa sana
2026-10-28 16:02:42
10
nestory mm :
KWA AJILI YA MATESO MAKALI YA BWANA WETU YESU KRISTU.
2026-10-28 17:11:56
6
zainabu :
mungu akulinde sana baba
2026-10-29 06:47:27
2
Deus Ndyamkama :
Sidhani kama watakuelewa.
2026-10-28 16:25:31
5
beatricerwizaa :
Asante baba
2026-10-28 19:47:00
3
Ernie,cute🥰 :
Mwenye masikio na asikie
2026-10-28 18:30:14
3
Magia mbilinyi :
Amina baba
2026-10-28 18:29:01
2
user3415904086017 :
Amen
2026-10-28 15:58:44
3
GASPER KISINZA :
WENGI SANA...Mungu AJE NA ALIPIZE KISASI CHAO
2026-10-29 12:01:54
0
It's 💫BRIELLA🥷💦💧 :
amina
2026-10-28 13:50:47
2
Japheth :
hasate. bababa.
2026-10-29 08:56:07
0
maria :
amin
2026-10-29 04:52:20
0
Francis Felician :
baba Padri ishi Miaka yote ukiwa unasema ukweli kama huu wenye masuki wamesikia
2026-10-29 11:34:04
0
akko :
kweli. kabisa. baba
2026-10-29 09:28:26
0
enjoy :
asantee baba
2026-10-29 07:21:51
0
innocent swai :
amen
2026-10-29 05:16:13
0
GGM Collection :
Ubarikiwe saana Babaa
2026-10-29 06:03:33
0
Nassibu Decor :
sielew
2026-10-29 17:33:56
0
abdul mussa :
Makanisani ndiyo mafundisho ayooo😂
2026-10-29 07:29:15
0
🥰 :
mbona enzi za mkapa watu wa hivi hawakujitokeza ?
2026-10-29 09:36:11
0
Ibrah msimbazi :
hii vita ya wakatoliki na rais ni kali sana😂😂😂
2026-10-29 05:54:49
0
abraham kahai :
🤣🤣🤣
2026-10-29 06:54:13
1
To see more videos from user @breezt4, please go to the Tikwm
homepage.