💔🕊️UJUMBE WANGU KWA POLISI
Kila tarehe hii ikifika, moyo wangu unaumia ninapomkumbuka mama yangu mdogo, aliyeuawa na polisi wakati wa maandamano.
Polisi, mnapaswa kuwa walinzi wa maisha ya wananchi, lakini familia yangu imebaki na maumivu ya kumpoteza mtu tuliyempenda. Je, nani atafuta machozi yetu? Nani atairudishia familia yetu maisha tuliyoyapoteza?
Mama yangu mdogo alikuwa na haki ya kuishi kama binadamu mwingine yeyote. Maisha yake yalikuwa na thamani, na hakuna siku nitakayoweza kusahau maumivu ya kumpoteza kwa namna hii.
Tunataka haki, ukweli na uwajibikaji. Maisha ya Mtanzania mmoja ni muhimu. Hatuwezi kuufuta uchungu huu, lakini hatupaswi kusahau thamani ya maisha ya binadamu.
Pumzika kwa amani, mama mdogo. Familia yako haitakusahau. 🕊️💔
2026-10-29 07:37:34
10
@kp😜_kemar78👑 :
Appreciate
2026-10-29 08:14:04
0
B 💥💥 :
tarehe 29 mwenzio wa 10 siwezi kuisaa yaliyo tokea
2026-10-29 07:10:36
12
Bakary mwandu :
nilitoka Sinza adi Tabata kimanga kwa mguu bila kuchoka Wala kumuliza mtu shot kat
leo police wapo kila kituo🥹
mwenyez MUNGU alaze roho zote za marehemu mahali pema pepon🕊️💔
2026-10-29 07:37:15
5
JOSEPH NGOWI :
basi tu sijui ni upepo gani ule.
Mungu tuepushe na hasira zitiazo hasara.
maumivu yale , kufutika .....
mlotangulia mpate tulizo jema🕊️tulohai tupate faraja zaidi .
2026-10-29 07:28:56
9
it's Sally💦🥀 :
kumbukumbu mbaya ambayo sitamani itokee tuliteseka sana jmniii uhuru wakweli ni makubaliano sio vurugu mungu ndo hakimu wa Kila jambo azipumzishe roho zilizokufa na Atupe Amani tuliohai😳
2026-10-29 07:18:01
8
BARAKA MTULIVU :
iyo bajaji mbn km plate namba yk ni mpya tena G kwaiyo hii ishu ni ya leo au
2026-10-29 07:37:56
7
hidday.mussa🦋 :
Sito sahau hii siku 😭💔🙌
2026-10-29 07:14:15
5
Allyliza :
Tanganyika yangu😭😭😭
2026-10-29 09:10:03
0
happy msuya :
daaah
2026-10-29 07:20:17
2
Miss designer 🔥🥀 :
Makombolelo 🥺
2026-10-29 08:00:49
1
rahma💔💓 :
hii siku ingekuwa yakihistoria kwakweli sitoisahau
2026-10-29 09:03:10
2
To see more videos from user @billy_brand25, please go to the Tikwm
homepage.