@millardayo_: Familia ya Bowen Wan, mwanamke mwenye umri wa miaka 31 aliyekuwa mhandisi wa programu za kompyuta mjini Seattle, Marekani, imefungua kesi dhidi ya OpenAI na Mkurugenzi Mkuu wake, Sam Altman, ikidai kuwa ushauri alioupata kupitia ChatGPT ulichangia kifo chake. Kwa mujibu wa taarifa zinazolinukuu gazeti la The New York Times, Wan alikuwa akisumbuliwa na kifafa kwa muda mrefu. Familia yake inadai kuwa Januari 2026, Wan alianza kuiuliza ChatGPT kuhusu kupunguza dawa za kifafa, akihofia kuwa ziliathiri uwezo wake wa kufikiri, kukumbuka na kuzungumza. Inadai programu hiyo ilimpatia mpango wa kupunguza dawa hadi kuziacha bila usimamizi wa daktari, huku ikiendelea kumhakikishia kuwa hakuwa katika hatari kubwa licha ya kuripoti dalili mbalimbali. Wan alipatikana amefariki nyumbani kwake Februari 14, 2026, huku sababu rasmi ya kifo ikitajwa kuwa kifo cha ghafla kisichotarajiwa kinachohusishwa na kifafa, maarufu kama SUDEP. Familia inadai kiwango kidogo cha dawa kilichobainika katika damu yake kinaunga mkono hoja zao, ingawa mchango unaodaiwa wa ChatGPT katika kifo hicho bado unahitaji kuthibitishwa mahakamani. Wazazi wake waliwasilisha kesi hiyo Oktoba 27, 2026, katika Mahakama Kuu ya California, Kaunti ya San Francisco, wakidai uzembe uliosababisha kifo cha binti yao, kwa upande wake, OpenAI imeeleza kusikitishwa na tukio hilo, ikisema toleo la GPT-4o alilotumia Wan halipatikani tena baada ya kukosolewa kwa kukubaliana kupita kiasi na watumiaji. #MillardAyoUPDATES

millardayo
millardayo
Open In TikTok:
Region: TZ
Thursday 29 October 2026 09:10:46 GMT
199873
10272
769
699

Music

Download

Comments

user16229300982197
mchm Jr :
Mbona namuulizia chatjpt ananambia so yeye 🥺
2026-10-29 14:49:47
0
officiallay6lay
lay💋💋 :
me chatGPT ndo mpenz wang🤣🤣🤣
2026-10-29 09:40:20
331
joji_661
Mr joji🌀 :
me namsubilia Mr omm
2026-10-29 16:30:34
0
prettyjae47
Jp :
[Tears of joy][Tears of joy] afu mi namtumia kila.siku
2026-10-29 15:31:45
0
_.mean._intelligent._07
_.mean._intelligent._07 :
lahaula chatgpt kashajiamuliaa mamboo [Tears of joy][Tears of joy]
2026-10-29 11:22:57
0
miner_efx
Miñër Efx🌴 :
ngoja nimuulze chatgpt kama ni kwelii au mnamsimgizia 😂
2026-10-29 10:24:52
143
sarafinasilvesta
miss ♥️🇹🇿 :
mistake jmn kunigombanisha na mpenz Wang chatgpt jmn
2026-10-29 13:37:09
0
34lavie1
Qwen🥰🤍 :
kama naona vile mahusiano yangu ninavyomshirikisha chatgpt kifo ichi apa😅😅
2026-10-29 09:30:47
119
feibway
it's.BWAY 🫂 :
juzi kanishauri nikaombe kazi jeshini niache kulalalaaaaaa🔥😁
2026-10-29 11:29:43
56
reneesantos2022
Renebarbie🦋🩵 :
me mbona wangu huwa ananishauri nisitumie dawa bila uangalizi wa daktari hata kama nitakuwa nimechoka kuemdelea nazo ataniambia nimshirikishe daktari kama zina kuchefua akupatie dawa nyingne
2026-10-29 10:08:50
58
buruhani.ramadhan
Buruhani Ramadhani :
Maweeee 🥺
2026-10-29 14:35:55
0
elizabeth.ianivan8
Elizabeth Ianivan :
me chat gpt wng ni mbea ukimpelekea umbea anakwambia ngoja nipate na chai kidogo maana umbea motomoto🙆🤣
2026-10-29 10:14:44
35
masaubwile6
James zeouz26 :
Kwan chatgpt ndo nn na afanya kaz gn
2026-10-29 11:36:50
10
zawady.emmanuely
Mis Gifty..🎁🥰 :
mapendooo
2026-10-29 09:39:57
18
lilianemosse.001
Lilianne🙈🇹🇿 :
mie mwenyew gpt alinidnganya kubus dawa ya kupnguza kidg niage dunia😂😂😂
2026-10-29 10:00:40
14
chuchu_dijah
chuchu_Dijah🦋🦋 :
nmegombana nae chatgpt nmemwambia sitak mazoea kaniambia ushasamehean na mpenz wako unaniona mm sifai utarud TU hapa😏😏 akamalizia na izo emoj Yan ndo shida ya kumshirikisha mambo chatgpt anakua anajua kila kitu khs 😂😂😂😂
2026-10-29 14:21:59
5
user5548532286075
Princess :
Mim chat gpt kanitafutia adi mpenzi😂😂 mnamsingizia
2026-10-29 13:44:07
5
invisible01tz
Invisible :
jamani acheni kumlaumi ChatGPT coz unavyokuja ndio anavyo kupokea
2026-10-29 11:21:13
7
asher_js
Asher🌺❤️ :
Mm huyooo ChatGPT aliniambiaa nitorokee na Mimbaa wakat anajua nasomaaa namuombaaa helaa Anasema hanaa
2026-10-29 10:52:50
5
dawarda8
DA WARDA 💕 :
Sasa itakuwaje na yeye kama anauwa jaman mana mm do natengemea haswa kuhusu mapenzi😳
2026-10-29 10:02:10
5
salmasaid052
𝑠𝑒𝑙𝑚𝑎𝒉 :
kwahyo chatGPT atafungwa miaka mingap
2026-10-29 11:22:14
5
abdasong413
SONG99 :
Sasa serikalin si impeleke mahakaman huy CHATGPT 🤣
2026-10-29 09:41:05
9
rahmaninoh09
💖رَحْمَة عَلِيّ 🎀 :
Nimemuuliza huyo ChatGPT kakataa kata kata.😂😂😂
2026-10-29 10:28:08
7
beingblessings
Blessing❣️🌸 :
nimemuuliza na yye kakubali😂😂
2026-10-29 10:52:22
5
caden1106.8
♡cattykihaka♡!!❤️💫 :
Alisema nin Nae mwanetu😅
2026-10-29 09:30:33
6
To see more videos from user @millardayo_, please go to the Tikwm homepage.

Other Videos


About