@jambotv_: VIDEO: Mbunge wa Mtwara Vijijini, Arif Suleiman Premji, amehoji hatua za kikodi zinazochukuliwa na Serikali kukabiliana na kupanda kwa gharama za maisha, akitaka ufafanuzi kuhusu namna sera za fedha zinavyoweza kuhakikisha ukuaji wa uchumi unanufaisha wananchi moja kwa moja. Akiuliza swali Bungeni jijini Dodoma, Premji amesema licha ya Serikali kueleza kuwa uchumi wa nchi unaendelea kukua, takwimu za Fahirisi ya Bei za Taifa (NCPI) za Septemba zinaonyesha ongezeko la fahirisi hiyo kutoka 119.86 hadi 125.07, hali inayoibua maswali kuhusu uwezo wa wananchi kumudu gharama za bidhaa na huduma. Amesema hali hiyo inahitaji mikakati madhubuti ya kikodi na sera za fedha zinazolenga kudhibiti ongezeko la bei na kupunguza mzigo wa gharama za maisha kwa wananchi wa kawaida. Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Fedha, Mshamu Ali Munde, amesema Serikali inatambua athari za mabadiliko ya gharama za maisha na inaendelea kuweka sera, sheria na kanuni zinazolenga kudhibiti mfumuko wa bei. Munde amesema mfumuko wa bei nchini bado uko katika tarakimu moja, kati ya asilimia tatu na tano, kiwango alichosema kinaifanya Tanzania kuwa miongoni mwa nchi zinazofanya vizuri katika eneo hilo barani Afrika Mashariki. Amesisitiza kuwa Serikali itaendelea kuboresha sera na mifumo ya usimamizi wa uchumi ili kudhibiti mfumuko wa bei na kupunguza athari zake kwa wananchi, hususan katika uwezo wao wa kununua bidhaa na huduma muhimu.
Jambo TV
Region: TZ
Thursday 29 October 2026 15:19:32 GMT
Music
Download
Comments
ThomasSG :
teteeni na madiwani diwani ana posho ya laki tatu tu kwa mwez wala hakumbukwi
2026-10-29 15:31:17
0
To see more videos from user @jambotv_, please go to the Tikwm
homepage.