@uhondo.tv: Wanafunzi wanane wanaodaiwa kuwa wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST) wanashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya kwa tuhuma za kuwafanyia mitihani wanafunzi wengine wa Chuo cha Ufundi Moravian jijini Mbeya, inayosimamiwa na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET), kwa malipo ya Sh 100,000 kila mmoja. Tukio hilo linadaiwa kuhusisha mitihani ya fani ya Umeme wa Majumbani Daraja la Tatu (Electrical Installation Level Three), ambapo watuhumiwa wanadaiwa kufanya mitihani hiyo kwa niaba ya wanafunzi wengine kwa lengo la kujipatia fedha. Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya, chini ya Kamanda wake SACP Benjamin Kuzaga, linaendelea na uchunguzi kubaini mazingira halisi ya tukio hilo pamoja na kuwabaini wahusika wengine wanaoweza kuhusika. Hata hivyo, tuhuma hizo zinapaswa kuthibitishwa kwa mujibu wa sheria, huku watuhumiwa wakichukuliwa kuwa hawana hatia hadi pale mahakama itakapothibitisha vinginevyo. #UhondoTVUPDATES
Uhondo TV
Region: TZ
Friday 30 October 2026 14:05:28 GMT
Music
Download
Comments
KATCO :
MUST home of Engineering
2026-10-31 03:46:41
0
Wilsoni Samweli :
hatar
2026-10-30 14:10:25
0
Nestory Magesa :
Must tyutengwe duuu VIPANGA NI WENGI SANA had vyuo vingine mmeend kuwafanyia mitihani
2026-10-30 15:36:39
0
To see more videos from user @uhondo.tv, please go to the Tikwm
homepage.