@almecky_tz: Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imetangaza kupandisha vima vya chini vya mishahara kwa wafanyakazi wa sekta binafsi, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuboresha maslahi ya wafanyakazi na kukabiliana na gharama za maisha. Akizungumza na waandishi wa habari Zanzibar, Waziri wa Kazi, Ajira, Vijana na Uwezeshaji, Ali Suleiman Mrembo amesema hatua hiyo imekuja baada ya Wizara kupitia Kamisheni ya Kazi na Bodi ya Ushauri ya Mishahara kufanya mapitio ya viwango vya chini vya mishahara katika sekta hiyo. Kwa mujibu wa viwango vipya vilivyotangazwa, wafanyakazi wenye mikataba ya maandishi katika taasisi za sekta binafsi watalipwa shilingi 450,000 kwa mwezi kutoka shilingi 347,000 za sasa, huku wafanyakazi wa taasisi ndogo zilizoainishwa katika kanuni wakipandishiwa kutoka shilingi 250,000 hadi shilingi 300,000 kwa mwezi. Aidha, wafanyakazi wa kutwa wenye ujuzi watalipwa shilingi 35,000 kwa siku kutoka shilingi 30,000, wakati wasio na ujuzi watalipwa shilingi 30,000 kutoka shilingi 25,000 kwa siku. Katika kundi la wafanyakazi wa majumbani, wanaoishi katika nyumba za waajiri watalipwa shilingi 110,000 kwa mwezi kutoka shilingi 100,000, huku wale wasioishi katika nyumba za waajiri wakilipwa shilingi 130,000 kutoka shilingi 120,000 kwa mwezi. Kwa upande wa wafanyakazi wa kigeni, kiwango cha chini cha mshahara kimepandishwa kutoka dola za Marekani 1,000 hadi dola 1,500 kwa mwezi. Waziri Ameir amesema Serikali imetoa kipindi cha miezi mitatu kwa waajiri wa sekta binafsi kufanya maandalizi ya bajeti na kurekebisha mifumo ya mishahara kabla ya kuanza kutekeleza viwango hivyo kuanzia Januari mosi mwaka 2027. #Zanzibar #Tanzania #Habari #Football #Trending
almecky_tz
Region: TZ
Saturday 31 October 2026 12:40:07 GMT
Music
Download
Comments
donnamontan🧡 :
@North valley hospital
2026-10-31 17:02:38
0
Salama Juma :
Mahoteli yanaingia hapa??
2026-10-31 16:44:56
1
Bill Wonder 🚁 :
MUWE MNAFATILIA KWA WAFANYAKAZI KAMA AMRI IMEFANYIWA KAZI, SIO MNAONGEA TU HALAFU MNAACHA HIVYO HIVYO !!!
2026-10-31 15:19:54
14
heavenwilly225 :
zanzibar ipi kwanza hii hii au
2026-10-31 16:12:56
3
Salha Ramadhan :
na sisi tusio fanya kz serekalini vp ss mumetufikiria ?
2026-10-31 14:35:20
4
Ibrahim Bernard :
serikali ya zanzibar haipo seriously kwenye sheria ya wafanyakazi binafsi sheria wanaziweka lakn hazifuati wana kula rushwa tu nawakati kuna hotel kibao wafanyakazi hawana mikata wananyanyasika kazini na wajiri wao .wazungu wanasaminiwa sana waonapewa mishahara mikubwa😭😭😭
2026-10-31 17:24:31
1
Jamaldin :
kuongeza mishahara mnayafanya maisha yazidi kua magumu shusheni ushuru bidhaa zishuke bei ndio kumrahisishia mwananchi ugumu wa maisha msahara Tsh 450,000 sukari inatoka kwenye Tsh 3000 inakwenda Tsh 5000 mafuta ya kula yanatoka Tsh 3000 kwa lita yanakwenda Tsh 5000 je hapo mshahara huo bado maisha yanazidi kua magumu kwa aliekua hana mshahara tunaomba shusheni maushuru ya kila sehemu ilimrqhisishe maisha kwa wote.
2026-10-31 13:42:36
2
official mush🕸️buibui junior :
mbna uku bala kumepowa yani uku tunapelekwa kama mbuzi tu
2026-10-31 17:04:13
0
bint mikidad :
ni vizur zikafuATILIWA HIZO SEKTA BINAFSI ITAPENDEZA SANA KUANGALIA AMRI INAVOFANYIWA KAZI
2026-10-31 16:25:47
0
sadry side :
musikimbilie sector binafsi kuongeza pesa na kama kiwango kinachoingia hakikidhi kuwalipa wafanyakazi wake hela izo je?
2026-10-31 17:39:07
0
Miss latty❤️ :
Ttz hawafati sheria
2026-10-31 17:09:20
0
AGS collection :
katika hilo inabid msimame hasa maana pesa tunazo ingiza ni nyingi mnoo kwa mahotel unakuta mtu unafanya kaz ngum unakuja kulipwa laki 3 serikali ismame
2026-10-31 16:53:36
1
Parchmy :
Bara shida nn jamn 😂😂😂
2026-10-31 17:18:35
0
Hidaya :
mungu awapekila lakher
2026-10-31 17:04:40
0
OMAR KHATIB :
INGALIKUWA MNAUZALENDO. WANANCHIWENU. BASIHAKUNAHAJAYAKUPANDISHA MSHAHARA. KWANI. MAISHA YAWANANCHI. NIHERIKUFA. ILOMNQLIJUWA. JUKUMU LENU NIKULIOKOWATAIFA. SIJENGINE.
LAKINI HAMTAKI USHAURI. WAWA NANCHIWENU.
2026-10-31 14:25:58
0
Bettina 🥰 :
jaman ongeren Kwa watu wa Zanzibar uku si tunateseka jaman na maisha ni magumu
2026-10-31 16:53:06
0
user3192059384552 :
hongera serekali yetu,tume elewa,ila hapo kwenye ongezeko la wafañya kazi wa majumbani ambao Wana ishi Kwa wajiria wawo mbona km ongezoko lao n dogo laki 1 had laki 110,
2026-10-31 14:49:02
1
eddymdosi1 :
sisii badoo atujapewaa
2026-10-31 13:32:21
2
Khalid Khelef :
mashallah
2026-10-31 15:40:32
0
LUNGU ٠٥٢٠ :
sio shida kuongeza lakini biashara zinasuasua
2026-10-31 15:45:12
0
muhan1730 :
Sekta binafs ni kam zip jaman?
2026-10-31 17:41:27
0
Devid kamata :
Kwaiyo na wale waliokuwa wakilipwa lak450
2026-10-31 16:01:16
0
zlatan :
mnatanga ila hukunhaiongezwi na hamfatiliii ktk hayo masecta binafsi hususan ktk haya mahospital binafsi ndio hawaongezi mm mke wangu ni muhanga wa hilo
2026-10-31 17:42:43
0
BADY❤ :
Mbna si tuna poke a ile ile laki 3 jmn 😭😭😭😭🥹🥹🥹🥹🥹😭😭😭😭 fatilieni jmn
2026-10-31 17:37:50
0
mrs mohd❣️💍🫂👩❤️👨❣️ :
asa wameongeza nn apo
2026-10-31 14:02:53
0
To see more videos from user @almecky_tz, please go to the Tikwm
homepage.