@smartvetwith_veronica: šŸ‚ KUNUNUA NG’OMBE WADOGO, KUWALEA MWAKA MMOJA NA KUWAUZA: JE, HUU NI MFUMO MZURI WA BIASHARA? Katika ziara yangu ya mnadani, nilipata nafasi ya kuzungumza na mtaalamu mwenzangu wa mifugo ambaye ameelezea mfumo wake wa biashara. Ananunua ng’ombe wadogo, anawatunza kwa takribani mwaka mmoja kwa mfumo wa uchungaji na lishe bora, kisha miezi miwili ya mwisho huwaongezea supplements ili kuboresha ukuaji na hali ya mwili kabla ya kuwauza. Pia tumeangalia tofauti ya kuchagua ng’ombe wadogo na wakubwa kwa ajili ya biashara ya kunenepesha. šŸ“Œ NG’OMBE WADOGO: Unanunua kwa lengo la kuwalea na kuwakuza kwa muda mrefu kabla ya kuuza. šŸ“Œ NG’OMBE WAKUBWA: Kwa biashara ya kunenepesha kwa muda mfupi wa siku 60–90, ni vizuri kuzingatia ng’ombe wenye umri wa takribani miaka 2–5, wenye afya nzuri na uwezo wa kuongeza uzito. Kumbuka, umri pekee hautoshi kufanya uchaguzi. Muonekano wa mwili, afya, historia ya lishe, aina ya ng’ombe na gharama ya ununuzi ni mambo muhimu ya kuzingatia. SWALI: WEWE UNGECHAGUA MFUMO UPI? 1. Kununua ng’ombe wadogo na kuwalea kwa mwaka mmoja? 2. Kununua ng’ombe wakubwa na kuwanenepesha kwa siku 60–90? Andika maoni yako hapo chini! šŸ‘‡ Unahitaji kuanza biashara ya kunenepesha ng’ombe lakini hujui pa kuanzia? Follow Smart Vet with Veronica kwa elimu, mafunzo na ushauri wa kitaalamu kuhusu biashara ya mifugo. Tunatoa huduma za ushauri na mafunzo ya kunenepesha ng’ombe ili kukusaidia kufanya maamuzi sahihi kabla ya kuwekeza. #SmartVetWithVeronica #KunenepeshaNgombe #BiasharaYaMifugo #CattleFattening #NgombeWaNyama

Smart Vet with Veronica
Smart Vet with Veronica
Open In TikTok:
Region: TZ
Saturday 31 October 2026 14:03:08 GMT
2956
110
15
10

Music

Download

Comments

user7035851838335
smart boy 06 :
hilo dume kubwa umesema bei gani
2026-11-01 06:41:24
1
carlos.mwakisole
Carlos Mwakisole :
namuona ndugu Moi😁
2026-10-31 22:23:17
1
tiger_style8
pk_officialtz :
hapo n wap vero
2026-10-31 14:54:42
1
user6190305304192
Karama :
Vero nko Bagamoyo kiromo,Mnada wa huku bagamoyo una uzoefu nao?
2026-10-31 16:38:07
1
williemnyamwezi
williemnyamwezi :
Vero njoo huku Kagera ng'ombe wa huku aina ya nyankole na Nyabugesela wanakuwa kwa speed nzuri pia wana bei nzuri baada ya kuwanenepesha na nyadi zipo kama utakuwa interested nicheck inbox tubadilishane uzoefu mi ndo nafanya hii biashara pia ni muajiriwa
2026-11-01 05:20:57
1
adellanzihekele1
adellanzihekele :
āœ…āœ…
2026-10-31 16:39:08
1
To see more videos from user @smartvetwith_veronica, please go to the Tikwm homepage.

Other Videos


About