@salome_donld: Usiruhusu hasira ikutawale mpaka ukasema maneno utakayokuja kuyajutia. Jifunze kusema kwa neema hata unapokosewa, jibu kwa hekima, na sema kwa upendo. Usitumie maneno yako kumvunja moyo mwingine. Kumbuka, wakati mwingine neno lako moja linaweza kuwa sababu ya mtu kupata nguvu ya kuendelea. Leo, kabla hujasema, muulize MUNGU akupe maneno yanayofaa. #ManenoYaHekima #UsivunjikeMoyo #TafakariKablaYaKusema #UjumbeMuhimu #maisha