@prophet_isaiah_mkailwa: ♦️AMKA KABLA HAIJACHELEWA! Usiilinde dini yako kuliko unavyotafuta wokovu wa roho yako! Sanamu haziwezi kukuokoa, miungu ya uongo haiwezi kukupa uzima wa milele, wala kila anayejifanya mtume hajatoka kwa Mungu hawezi kukupa uzima wa milele zaidi ya Yesu kristo peke yake. Acha ibada ya sanamu, geuka kutoka kwa miungu ya uongo, tubu dhambi zako, na umwamini Yesu Kristo peke yake. Dini haiwezi kuchukua nafasi ya toba, wala ibada za nje haziwezi kuokoa moyo usiogeuka kwa Mungu. Siku ya hukumu, hutahesabiwa haki kwa jina la dini yako, bali unahitaji wokovu ulio katika Yesu Kristo. Usisubiri hukumu ikufundishe kile ambacho Neno la Mungu linakuonya leo! “Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo.” — Matendo 4:12 🔥 YESU KRISTO NDIYE MWOKOZI. TUBU, MWAMINI, NA UOKOKE LEO! #YesuKristo #Toba #Wokovu #InjiliYaKweli
Isaiah_Mkailwa
Region: TZ
Sunday 01 November 2026 05:46:35 GMT
Music
Download
Comments
DR.MAJI MAREFU :
😂😂😂kumbe kwenye biblia maandiko yapo na Amsemi jaman mbona mnatuchanganya jaman
2026-11-01 06:45:16
0
To see more videos from user @prophet_isaiah_mkailwa, please go to the Tikwm
homepage.