@fastpromedia: Makamu wa Rais Deogratius Ndejembi ametoa wito kwa nchi Wanachama wa Ukanda wa Maziwa Makuu kuwapa wanawake nafasi yenye ushawishi katika maamuzi na mazungumzo ya amani. Akilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kufungua Mkutano wa Kwanza wa Kimataifa wa Wabunge Wanawake wa Nchi Wanachama wa Ukanda wa Maziwa Makuu -FP- ICGLR, unaofanyika Jijini Dar es Salaam. Amesema wanawake ni viongozi, wapatanishi na wajenzi wa amani ambao mchango wao unapaswa kupewa nafasi katika kuzuia na kutatua migogoro. Amesisitiza kuondolewa kwa mila kandamizi, ubaguzi na vikwazo vya kiuchumi vinavyo wanyima fursa huku akihimiza uwekezaji katika elimu, ujuzi na uchumi wa wanawake na vijana ili kujenga msingi imara ya usalama na maendeleo. Amesema utekelezaji wa Azimio Namba 1325 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa uonekane katika fursa halisi za maamuzi, elimu, ardhi, mitaji, teknolojia na ajira zenye staha. #tanzania #zanzibar #fpupdates

FP Media
FP Media
Open In TikTok:
Region: TZ
Monday 02 November 2026 16:03:40 GMT
3502
105
2
3

Music

Download

Comments

lincoln.a7
lincoln.A7 :
👏👏👏
2026-11-02 18:52:04
0
user432812993074
jeward thinks :
👍👍❤️❤️
2026-11-03 03:43:20
0
To see more videos from user @fastpromedia, please go to the Tikwm homepage.

Other Videos


About