@wakudata.msukuma: Leo Mahakama kuu ya Kenya imesikiliza kesi ya kutekwa kwa Mwanaharakati wa Tanzania, Twaha Mwaipaya jijini Nairobi mnamo tarehe 25 October 2026. Katika kesi hiyo Inspekta Jenerali wa Polisi nchini humo, Douglas Kanja, na Mwanasheria mkuu wa serikali waliburuzwa mahakamani hapo kueleza alipo Twaha. Polisi wamejitetea kwamba hawamshikilii Twaha na wala hawajui alipo. Hata hivyo pamoja na utetezi huo, Jaji wa Mahakama Kuu Alexander Muteti amemtaka IGP Kanja kueleza ni wapi alipo Twaha Mwaipaya ikiwa Polisi hawapo nae. Jaji Muteti amesema ni jukumu la Polisi kulinda raia na mali zao, hivyo kama hawamshikilii Twaha basi waseme anashikiliwa na nani. Kushindwa kufanya hivyo ni kushindwa kutekeleza wajibu wao kisheria. Katika kesi ya maombi ya Habeas Corpus inayotaka Mwaipaya afikishwe Mahakamani au mamlaka zieleze alipo, Jaji Muteti amelitaka jeshi la Polisi kuwasiliana na kampuni za simu ili kupata taarifa zinazoweza kusaidia kumpata Twaha. Hata hivyo Wakili wa Serikali Christopher Marwa, amesema tayari Polisi wameomba taarifa za Twaha kutoka kwenye mtandao aliokua anatumia, lakini bado mtandao huo haujawapa polisi taarifa hizo.!239
wakudata msukuma
Region: TZ
Monday 02 November 2026 17:57:14 GMT
Music
Download
Comments
🇨🇩🇰🇪Enock Maluli🇨🇩🇰🇪 :
Kenya 🇰🇪 juu
2026-11-02 20:13:11
2
user3175912903162 :
iyo ndio kenya ss kwetu huku utajuta
2026-11-02 21:24:03
1
RAYMOND Mwengwa :
sawa munguuu anajua sanaaaa.uzuri njia hyo 2
2026-11-02 21:22:59
0
George Zablon :
Kule malawi it was scam
2026-11-02 20:43:31
0
Ally Beko :
🥰🥰🥰
2026-11-02 19:12:24
2
To see more videos from user @wakudata.msukuma, please go to the Tikwm
homepage.