@jambotv_: VIDEO: Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bara, John Heche, amezitaka mamlaka zilizopo madarakani kutoka hadharani, kuomba radhi, na kulipa fidia kwa familia za waliouawa na majeruhi wa matukio ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025. Heche ameyasema hayo leo, Novemba 3, 2026, wakati akizungumza katika maadhimisho ya kumbukizi ya mwaka mmoja wa mauaji ya Oktoba 29, 2025, yaliyoandaliwa na chama hicho. Akiwasilisha msimamo wake kuhusu haja ya kuwa na ukweli, haki, na uwajibikaji, Heche amezisihi mamlaka kurudi nyuma mapema na kuweka wazi kilichotokea pamoja na waliohusika na matukio hayo. "Ni suala la muda tu kuendelea kuwakandamiza Watanzania, Watanzania hawatakubali kamwe. Na mimi natumia nafasi hii usiku wa leo kuwasihi warudi nyuma ingali mapema. Moja, watoke hadharani waombe radhi”, ameeleza Heche. Heche ameeleza kuwa wananchi wamebaki na majeraha makubwa huku wengine wakiishi na risasi mwilini kutokana na matukio ya Oktoba 29, 2025.

Jambo TV
Jambo TV
Open In TikTok:
Region: TZ
Tuesday 03 November 2026 20:21:51 GMT
2024
105
5
1

Music

Download

Comments

vicent.bolt.nuts
vicent bolt nuts :
wana siasa hacheni kuhambia watu wahandamane ili mtuibihe,
2026-11-03 21:00:57
1
josephathmbwilo5
Josephmodoks :
uko sahihi kiongozi
2026-11-03 22:55:23
1
francsidamas
Francsi Damas :
amen ❤️🙏
2026-11-04 02:19:56
0
furenckmporogom1
Ef key 🗝️ :
🔥🔥🔥
2026-11-03 20:29:47
1
kulwa.ntugwa
kulwa ntugwa :
✌️
2026-11-03 20:35:32
1
To see more videos from user @jambotv_, please go to the Tikwm homepage.

Other Videos


About