@motherchildwellness1: Huyu ni mtoto aliyezaliwa na manjano (Neonatal Jaundice). Manjano makali husababishwa na kuongezeka kwa bilirubin kwenye damu. Yasipotambuliwa na kutibiwa mapema, yanaweza kuathiri ubongo na mfumo wa neva, na kusababisha changamoto zifuatazo: Utindio wa ubongo (Cerebral Palsy). Viungo kulegea au kukakamaa. Shingo kutokaza. Kuchelewa kukaa, kutambaa au kutembea. Misuli kuwa dhaifu. Degedege. Changamoto za kusikia na kuona. Kuchelewa kwa ukuaji na maendeleo ya mtoto. Ninasaidia watoto wenye changamoto za ukuaji kupata tathmini na mwongozo unaofaa. 📞 Dr Geaz: #jaudince #childcare #AfyaYaMtoto