@stormfmtz: Mbunge wa Mwibara, Kangi Lugola, amependekeza kufanyiwa marekebisho sheria ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ili kumpa mamlaka zaidi ya kukusanya ushahidi wa wizi, ubadhirifu na ufisadi, pamoja na kuwasilisha majalada ya uchunguzi kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP). Akichangia hoja Bungeni leo, Novemba 4, 2026, Lugola amesema licha ya CAG kubaini vitendo vya ubadhirifu na ufisadi kupitia ukaguzi, hatua dhidi ya wahusika hazichukuliwi ipasavyo kwa kuwa majukumu yake huishia kufanya ukaguzi na kuwasilisha taarifa kwa Rais. Ameeleza kuwa kuimarisha mamlaka ya CAG kutasaidia kuhakikisha ushahidi wa makosa yanayobainika unafikishwa kwa mamlaka za mashtaka ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa. #stormupdates #sautiyageita #storm #geita

stormfmtz
stormfmtz
Open In TikTok:
Region: TZ
Wednesday 04 November 2026 16:36:57 GMT
7246
152
2
1

Music

Download

Comments

suzan.laurence3
Suzan Laurence :
Kangi ni mmoja tu mwibara moja hiyo
2026-11-04 19:51:09
1
pallanyo01
Pallanyo@01 :
😁😁😁
2026-11-04 18:48:36
0
To see more videos from user @stormfmtz, please go to the Tikwm homepage.

Other Videos


About