@rashidbattashy: INFINITY YAANZA UJENZI WA MRADI WA DOLA MILIONI 50 KIKWAJUNI KWA MJERUMANI ✍🏻 @rashidbattashy Kampuni ya @infinitydevelopmentsofficial imeanza rasmi utekelezaji wa mradi mkubwa wa makazi ya kisasa katika eneo la Kwa Mjerumani, Kikwajuni Zanzibar, unaotarajiwa kugharimu takribani dola za Marekani milioni 50, sawa na shilingi bilioni 132.3 za Tanzania, huku ukitarajiwa kukamilika ndani ya miaka miwili. Ndani ya siku 30 tangu kukabidhiwa eneo hilo, kampuni hiyo imefanikiwa kusafisha eneo la mradi, kubomoa majengo ya zamani, kuondoa vifusi na kuanza uchimbaji wa misingi ya majengo, hatua inayoashiria kuanza kwa utekelezaji wa mradi huo kwa kasi. Akizungumza Novemba 5, 2026, Mwenyekiti wa Infinity Developments, @samuelsaba , amesema kampuni hiyo imejipanga kuhakikisha mradi unatekelezwa kwa ubora na kukamilika kwa wakati, kwa kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar pamoja na Shirika la Nyumba Zanzibar. Amesema kwa sasa kazi inaendelea katika uchimbaji wa misingi ya vitalu vinne, ambayo inatarajiwa kukamilika ndani ya siku 30 hadi 45. Mradi huo unatarajiwa kuwa na majengo ya makazi ya kisasa, eneo la biashara, pamoja na shule ya kimataifa ya GEMS International yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 1,500 kuanzia elimu ya awali hadi kidato cha sita. Katika kuhakikisha wananchi waliokuwa wakiishi eneo hilo hawanufaiki kwa kuondolewa pekee, mradi huo pia umejumuisha ujenzi wa nyumba 59 za fidia kwa kaya zilizohamishwa kutoka eneo la Kwa Mjerumani. Nyumba hizo zitakuwa na vyumba vitatu vya kulala, chumba kimoja cha mfanyakazi na zitakabidhiwa zikiwa zimekamilika pamoja na samani zote, huku wananchi hao wakitarajiwa kurejea katika makazi yao mapya ndani ya mwaka mmoja. Akizungumza wakati wa ziara ya Kamati ya Miundombinu, Ardhi na Tehama ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Mwenyekiti wa kamati hiyo, Mihayo Juma N’hunga, amesema kamati imeridhishwa na kasi ya utekelezaji wa mradi huo na itaendelea kuufuatilia kila baada ya miezi mitatu hadi minne ili kuhakikisha unakamilika kwa viwango vinavyotakiwa. Amesema wananchi waliohama wamepewa fedha za kodi ya pango kwa kipindi cha miaka miwili na Serikali wakati wakisubiri kukamilika kwa nyumba zao mpya.

Rashid battashy
Rashid battashy
Open In TikTok:
Region: TZ
Thursday 05 November 2026 17:32:13 GMT
3710
139
2
28

Music

Download

Comments

icy_hot225
icy_hot :
laundry room
2026-11-06 02:05:47
0
icy_hot225
icy_hot :
wawekeeni na laundry rooms, vyumba maalum vya kufulia, machine za kufulia na kukaushia.. au watafua varanda, maji yatachirizika.. nyumba zitaanza kuoza.. nyumba za wenyetu za kisasa zina laundry room
2026-11-06 02:05:19
0
To see more videos from user @rashidbattashy, please go to the Tikwm homepage.

Other Videos


About