@thanhloim: ip tieu su

Trương Thanh
Trương Thanh
Open In TikTok:
Region: VN
Friday 06 November 2026 16:30:00 GMT
43
5
0
2

Music

Download

Comments

There are no more comments for this video.
To see more videos from user @thanhloim, please go to the Tikwm homepage.

Other Videos

Kuna wakati katika maisha unafika mahali unakosa maneno ya kuelezea kile ambacho moyo wako unakihisi. Leo imekuwa moja ya siku hizo ambazo sitazisahau kamwe. Sikutarajia kwamba siku yangu ya kawaida ya kazi ofisini ingebadilika na kuwa siku iliyojaa mshangao, hisia nzito na machozi ya furaha.  Raya Hamad, Kulthum Masoud, Seif Mohamed, Rashid Ali, Mulhat Yussuf na Muumin Mwinyi,nyinyi watu wangu, mmenifanyia nini leo? Mpaka sasa sijui nani aliyewakusanya na kupanga mshangao huu, lakini ninachojua ni kwamba mmegusa sehemu ya ndani kabisa ya moyo wangu. Mmefika ofisini kwangu kwa kunishtukiza, mkiwa na zawadi na upendo mkubwa, kunipongeza kwa kutimiza mwaka mmoja wa uongozi wangu. Kilichonigusa zaidi si zawadi mlizoniletea, bali ni upendo, muda na thamani mliyonipa katika mioyo yenu. Kila mmoja wenu ana historia ya kipekee katika maisha yangu. Kila mmoja amenigusa kwa namna yake, na pengine hamjui ukubwa wa nafasi mlizonazo katika maisha yangu. Mmeongeza kumbukumbu nyingine nzuri ambayo nitaibeba moyoni mwangu siku zote.  Kuna watu unaokutana nao katika maisha na kupita, lakini kuna watu Allah anakukutanisha nao ili wabaki kuwa sehemu ya historia yako, furaha yako na nguvu yako. Nyinyi ni miongoni mwa zawadi hizo za thamani ambazo Allah amenijaalia. Leo mmenikumbusha kwamba mafanikio ya kweli si vyeo, nafasi wala madaraka pekee, bali pia ni kuwa na watu wanaokupenda kwa dhati na wanaofurahia mafanikio yako kana kwamba ni yao wenyewe. Nimejiuliza mara nyingi, hivi nimefanya nini kustahili upendo wote huu? Sina jibu zaidi ya kusema Alhamdulillah. Nimejaribu kutafuta maneno ya kuwashukuru, lakini kila neno linaonekana dogo mbele ya ukubwa wa kile mlichonifanyia. Mmeniliza, mmenifurahisha, mmenipa nguvu mpya na zaidi ya yote mmenifanya nijisikie kupendwa kwa namna ya kipekee sana. Mwaka mmoja wa uongozi umenifundisha mengi, lakini leo nyinyi mmenifundisha somo jingine kubwa kuhusu maana halisi ya urafiki, utu na upendo wa kweli. Asanteni kwa kunipenda, kunikumbuka, kunithamini na kuwa sehemu ya safari yangu. Sijui niseme nini tena, ila nawapenda sana Alhamdulillah for one year of leadership, and Alhamdulillah for the beautiful souls Allah has placed in my life.❤️

About