@mr_mangapi: USIISHI KWENYE MAFUNUO YA WENGINE 📌 📌 👇👇 Ufunuo wa Yohana 1:1 [1]Ufunuo wa Yesu Kristo, aliopewa na Mungu awaonyeshe watumwa wake mambo ambayo kwamba hayana budi kuwako upesi; naye akatuma kwa mkono wa malaika akamwonyesha mtumwa wake Yohana.... || [4]Yohana: "kwa yale makanisa saba yaliyoko Asia" Neema na iwe kwenu na amani, zitokazo kwake yeye aliyeko na aliyekuwako na atakayekuja; na zitokazo kwa roho saba walioko mbele ya kiti chake cha enzi.... Moja ya hatari kubwa katika maisha ya kiroho ni kufundishwa kitu bila kufundishwa namna ya kukichunguza, kukitafsiri na kuelewa muktadha wake. Kitabu cha Ufunuo kiliandikwa kwa muktadha maalumu, kikielekezwa kwa makanisa saba yaliyokuwa katika eneo la Asia Ndogo, ambalo kwa sehemu kubwa ni Uturuki ya sasa. - Efeso - Smirna - Pergamo - Thiatira - Sardi - Filadelfia - Laodikia Lakini leo unaweza kukuta mtu anafundishwa kwamba kila kitu kilichoandikwa katika kitabu hicho lazima akitafsiri moja kwa moja katika maisha yake, bila hata kujiuliza kilikuwa kinazungumzia nani, lini na kwa sababu gani. Ndiyo maana unaweza kukuta mtu anakuwa mateka wa hofu kwa sababu ya namba (666) mpaka namba hiyo inapojitokeza katika mazingira ya kawaida ya maisha, anaiona kama ishara ya nguvu za giza! Tatizo si kusoma Biblia, tatizo ni kusoma bila kuelewa muktadha. Unaposoma maandiko, jifunze kujiuliza maswali haya 📍📖 1. Nani aliandika ujumbe huu? 2. Aliuandika katika kipindi gani? 3. Aliwaandikia watu gani? 4. Kwa sababu gani aliandika ujumbe huu? 5. Ujumbe huu una maana gani katika mazingira yake ya awali, na una fundisho gani kwangu leo? Paulo aliwaombea waamini wapewe roho ya hekima na ufunuo ili wasiishi Katika Mafunuo ya Wengine! USIWE MATEKA WA MAFUNDISHO. KUWA MTU WA UFahamu! KINGDOM PLATE "Ufalme Uko Hapa" 💫 Unataka Ushauri au Mentorship au Darasa Maalumu la Mambo ya Kiroho, Unaweza Ukawasiliana nami Kupitia Whatsapp No +255 719 260 104 📱 Mr Mangapi......✍️ #trendingvideo #goviral #africantiktok #flypシ #videoviral
𝗠𝗥 𝗠𝗔𝗡𝗚𝗔𝗣𝗜
Region: TZ
Saturday 07 November 2026 05:03:10 GMT
Music
Download
Comments
MFUMO KRISTO :
BIBLIA NZIMA SIO KITABU CHA WAKRISTO NIKITABU KWA AJILI YA WANADAMU WOTE
2026-11-07 08:20:12
0
diva12 :
kila kitabu kwenye bibilia kipo kwa ajili ya ulimwengu mzima na sio watu fulani..soma maandiko kaka.
2026-11-07 08:16:56
6
Mobile Church Tanzania :
1.Wakorintho (1Co) 10:11 Basi mambo hayo yaliwapata wao kwa jinsi ya mifano, yakaandikwa ili kutuonya sisi, tuliofikiliwa na miisho ya zamani.
"Now all these things happened unto them for ensamples: and they are written for our admonition, upon whom the ends of the world are come."
2026-11-07 08:23:12
0
Scissor :
Unaposema haiwahusu waafrika hata injili yenyewe haikuja kwa ajili ya waafrika bali Israel,maana tunaemuomba ni Mungu wa Israel kama alivyojitambulisha tangu tangu na tangu,
Huku afrika na Amerika ni neema TU imetufikilia .
lakini unachopaswa kujua biblia hiyo hiyo imebeba matukio yaliyokwisha tokea na Yale yatakayokuja baadae.(Hadith na nabii)
lakini Mungu Bado anazungumza na watu wake hivyo kufundisha aliyokwisha kutenda Mungu na Yale atakayotenda Mungu bila kuangalia alitenda wapi au ataenda wapi kunafanya kizazi cha neema ambaccho ni afrika na America kiamini Mungu yupo alitenda,anatenda na atatenda.
2026-11-07 06:39:22
5
SON OF MAMA ONE. J_KIMARIO🇹🇿 :
What are you say!!
2026-11-07 12:29:56
0
ShimbaA :
vipi kuhusu barua za Mtume Paulo kwa Waefeso, Wafilipi, wakolosai etc, Sisi waafrika tuvisome?
2026-11-07 07:39:53
1
miriam minja :
kwan rais akihutubia wa singida ile hotuba haiwi ya taifa zima kwa kukosa maarifa ya roho wa Mungu
2026-11-07 08:57:19
1
Donatus Bernard Nyamizi :
kama ni hivyo, mbona uturuki asilimia kubwa ni waislamu
2026-11-07 07:04:17
0
Quantum _Vibe :
kwanza ufunuo ukisoma yote utachanganyikiwa kabisa😊 bila tafsiri sahihi ufunuo itakupoteza sana
2026-11-07 07:22:17
0
Marney hairstylish :
yeah..watu hawajui siri ya hizi namba tu. Shetani hana jipya.. anacopy tu
2026-11-07 05:49:31
0
mimi :
Kila andiko lenye pumzi ya Mungu lafaa kwa mafundisho.
2026-11-07 11:18:14
1
IPCharles :
bro hapa kinachotakiwa ni kuchukua ujumbe uliomo ndani ya ujumbe changamoto zilizotajwa kwenye makanisa hayo ndiyo changamoto zilizomo ndani ya watu waliomo makanisani
2026-11-07 07:17:48
1
Joff Mulenga :
Mafundisho hayo si sahihi kibiblia. Ni kweli kwamba makanisa saba yaliyotajwa katika kitabu cha Ufunuo yalikuwa Asia Ndogo, katika eneo ambalo leo ni Uturuki, lakini hilo halimaanishi kwamba kitabu hicho ni cha watu wa Uturuki pekee.
Ufunuo 1:3 inasema: “Heri asomaye, na wao wayasikiao maneno ya unabii huu, na kuyashika yaliyoandikwa humo...”
Pia, Ufunuo 22:16 Yesu anasema kwamba alimtuma malaika wake kutoa ushuhuda wa mambo hayo kwa ajili ya makanisa.
Kwa hiyo, ujumbe ulielekezwa kwa makanisa saba ya wakati huo, lakini Neno la Mungu linafundisha na kujenga kanisa la Kristo katika mataifa yote, ikiwemo Afrika na Tanzania.
Biblia haijagawanywa kwa misingi ya mabara au mataifa. Hatuwezi kusema kitabu fulani cha Biblia ni cha watu wa eneo fulani kwa sababu tu matukio yake yalitokea huko.
2026-11-07 12:23:05
0
Royal Priest :
Kwa mara ya kwanza nimeona umeongea upotofu
2026-11-07 13:05:40
1
Recho :
alie kutuma mwambie amechelewa sana
2026-11-07 12:19:12
0
Innocent Mndeme :
kaka hap0 nakupinga kitabu cha ufunuo kilizungumzia makanisa saba kwasababu ndio yaliyokuwepo. pale kitabu cha ufunuo kimeandika mataifa yote yatakusanyika mbele za bwana na hapo waliondikiwwa akina nani?
2026-11-07 11:48:04
0
Innocent Mndeme :
nlichogundua kila mtu kwenye mtandao kila mtu anaibuka cha kwake
2026-11-07 11:48:59
0
Donatus Bernard Nyamizi :
je hayo makanisa saba ya waefeso yapo? na kama hayapo sasa huo ujumbe kwa makanisa hayo lini utatimia
2026-11-07 07:05:53
0
Gedeon Maleka :
sasa tafsiri sahihi ni ipi?
2026-11-07 08:49:23
0
@Avin :
big up bro maana una maarifa yalio kuweka huru
2026-11-07 08:42:13
1
chanceombiza :
2026-11-07 11:10:33
0
Jemz70 :
Usitudanganye
2026-11-07 10:25:58
0
Gedeon Maleka :
na ya kushangaza eti iko n'a tafsiri 80
2026-11-07 08:49:03
0
user82904515078173 :
kabisa
2026-11-07 13:02:39
0
chanceombiza :
2026-11-07 11:10:36
0
To see more videos from user @mr_mangapi, please go to the Tikwm
homepage.