@sampala_farming: MAFANIKIO NI SIRI. Siri ya mafanikio kwenye kilimo ni kuwa na Elimu kuhusu kitu unahitaji kufanya ilikusudi ufanikiwee. Watu wengi huwa na picha ya mafanikio lakini hawajui wafanye nini ilikusudi waweze kufikia taswira ile ya mafanikio. Wataalamu wengi wenye ujuzi na maarifa ya mafanikio huwa tunakuwa hatujapata bahati ya kukutana na mtu mwenye kuweza kushirikiana nae kutuwezesha sisi kutimiza malengo yake. Siku zote malengo yetu huwa ni madogo lakini malengo ya Boss huwa ni makubwa. Watu wengi ambao wako vizurii kiuchumi huogopa kuwekeza kwasababu ya kukosa wataalamu wa uhakika watakaolinda rasilimali zisipotee. Tunaweza kufanya kazi bora na kuendesha miradi ikafanikiwa Kwa kushirikiana. Siri ya mafanikio kwa wakulima na wafugaji ni kuacha UBINAFSI. Tukipeana maarifa adimu sote tunaweza kufanikiwa.