@jambotv_: VIDEO: Mwananchi mmoja aliyejitokeza mbele ya Waziri Mkuu wa Tanzania Dkt. Mwigulu Nchemba, ametoa kilio chake kuhusu kero za huduma za afya, ukosefu wa nidhamu kwa baadhi ya watumishi wa umma, pamoja na madhila mengine aliyoyapata katika maisha yake. Tukio hilo limetokea leo, Novemba 7, 2026, wakati Dkt. Mwigulu akizungumza na wananchi katika Viwanja vya Polisi Mwandoya, vilivyopo Jimbo la Kisesa, akiwa kwenye ziara ya kikazi mkoani Simiyu. Akieleza kero yake mbele ya Waziri Mkuu, mwananchi huyo amebainisha kuwa amekuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa henia kufuatia kupigwa, lakini alipokwenda hospitalini Bariadi kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji baada ya kupewa rufaa kutoka Mwandoya, alikutana na urasimu pamoja na usumbufu kutoka kwa daktari, hivyo kumuomba Waziri Mkuu kufikisha ujumbe kwa Rais ili kurejesha nidhamu miongoni mwa watumishi wa umma. Mwananchi huyo ameongeza kuwa alivamiwa dukani kwake na kukatwa panga kichwani, na baada ya kufanya jitihada binafsi za kumkamata mtuhumiwa, mtuhumiwa huyo aliachiwa kwa dhamana. “Baadaye mtuhumiwa akadhaminiwa akawa nje. Nilivyoenda kwa Mkuu wa Wilaya ananiuliza: 'dogo haujafa? Yaani kakesi kadogo unafuatilia?”, ameeleza mwananchi huyo. Waziri Mkuu amebainisha kuwa ingawa vyombo vya ulinzi na usalama vinafanya kazi nzuri na kulinda amani ya nchi, makosa ya mtu mmojammoja hayapaswi kuchukuliwa kama taswira ya taasisi nzima. Amemwagiza Mkuu wa Mkoa na Jeshi la Polisi kufanya ufuatiliaji wa kina wa tuhuma hizo ili kubaini ukweli wa shambulio hilo na hatua zilizochukuliwa dhidi ya mtuhumiwa aliyeachiwa.
Jambo TV
Region: TZ
Saturday 07 November 2026 14:16:35 GMT
Music
Download
Comments
Shop with geelux 🛍️👗👡 :
Najivunia kuwa mkurya
2026-11-07 16:56:34
31
rufina lyimo :
huyu ni wangu mtu asimguse
2026-11-07 16:34:07
14
Dr.Engineer :
Huyubninmteja wetu WA MILEMBE
2026-11-07 15:47:37
12
Baba Hellena 2026 :
mmmmh hilaa hiiii nchiiiiii himeshauzwaaaahaaaa kwa kweli basiiiii😃😃😃😃😃🤣
2026-11-07 19:45:20
0
Minnah muddy@68 :
Hii taarifa Huwez ona Millard ayo ameipost😂
2026-11-07 18:42:14
5
masoo.com :
Kwani uyu katokea wapi jamani🥺
2026-11-07 17:20:40
4
Rider King :
my brother ana IQ kubwa sana [Pray][Pray] bigup
2026-11-07 16:26:48
7
isaya Joel :
sauti kama ya magufuli
2026-11-07 19:10:45
1
Kurian Disciple🇰🇪🇹🇿 :
I love the spirit we have as Kurians
2026-11-07 18:13:11
2
Nyakafwinda :
mara hatoki fara jamani wambie ukwer kak
2026-11-07 17:09:58
12
Buthaynah :
Ila watu dahh wanamaumivu sanaa kiukwel
2026-11-07 15:02:52
27
Likoteho daughter :
Dokta hawezi kuzuia kifo
2026-11-07 18:45:17
1
Tony :
hawana jipya hao wanasubilia utafute haki wakuone mmbaya na kukuteka
2026-11-07 19:33:58
1
mosani mitumbaTZ :
ameongea point
2026-11-07 16:46:13
6
Chalamila store :
mpen maiki yenye sauti jamani🥰🥰🥰
2026-11-07 16:22:07
9
lizzy 45 :
Anaongea yey naogopa mim 🥺🥺
2026-11-07 18:39:49
2
muba mziguq :
mim nilikabwa nika enda polis wanatak alabii 10000 halafu kuchua defenda hela nyengine nika samehe
2026-11-07 19:18:37
0
☠︎𝐌𝐢𝐠𝐮𝐞𝐥☠︎ :
Ila huyuu
2026-11-07 14:48:25
3
Erry erry :
tumuombee tu uyu
2026-11-07 15:12:00
4
YEKU S KEIYA🇹🇿🇹🇿 :
watu wana machungu
2026-11-07 16:37:11
3
janes sinyoramukure 👞 👠 :
🤣🤣🤣🤣🤣🤣usiniambie niende Arakawa ni ndoto ya kila mtu kuwa huru
2026-11-07 18:37:33
2
@Kurwasuit designer :
Niseme nisisemee..
2026-11-07 17:02:43
2
G.luck :
nawakumbusha tuu uyu ni babayangu mzazi kabisa🥰
2026-11-07 17:01:18
2
Jeijaa :
Watu wenye AKILI NDO WATAMUELEWAA
2026-11-07 17:06:36
1
To see more videos from user @jambotv_, please go to the Tikwm
homepage.