@mwanaspoti: Waziri wa Fedha wa Tanzania balozi Khamis Mussa Omar, ambaye anafahamika zaidi kwa majukumu yake ya Waziri wa Fedha yanayomweka mstari wa mbele katika masuala ya uchumi na sera za kifedha, ana upande wa pili wa maisha yake unaotawaliwa na mapenzi makubwa kwa michezo, hasa soka la Ligi Kuu England akiishabikia Arsenal, huku pia akiwa na mahaba kwa klabu ya Barcelona ya Hispania. Balozi Omar amekuwa mtetezi mkubwa wa mafanikio na historia ya Arsenal, akijivunia hadhi ya klabu hiyo na kuamini kuwa ina uwezo wa kuendelea kutawala soka la England kwa misimu mingi ijayo baada ya kurejea kileleni kufuatia kusubiri kwa miaka 22. #SourceNiSisi #mwanaspotiupdates #tunawezeshataifa