@jambotv_: VIDEO: Padri Lawrance Lukumay wa Parokia ya Mtakatifu Theresia amesema katika kipindi cha msiba ni muhimu familia na waumini kumtegemea Mungu, huku wakishikilia haki, amani na uaminifu katika maisha yao. Akizungumza leo Novemba 8, 2026, wakati wa ibada fupi ya kumuaga marehemu Mzee Alute Mughwai Lissu iliyofanyika nyumbani kwake jijini Arusha, Padri Lukumay amesema marehemu aliendelea kutamani kuona haki ikitendeka, amani ikiwepo na watu wakifuata taratibu hata wakati afya yake ilipokuwa ikidhoofika. Amesema marehemu alitumia maisha yake kutumikia jamii kwa uaminifu, akiwataka waumini kutumia vizuri akili na uwezo waliyopewa na Mungu katika kulitumikia taifa na jamii kwa haki. Padri Lukumay pia ametoa pole kwa familia ya marehemu, akieleza kwa namna ya pekee maumivu ya Tundu Lissu, mdogo wa marehemu, ambaye ameshindwa kushiriki mazishi ya ndugu yake kutokana na kuwa gerezani. Amesema Tundu Lissu angependa kuwepo katika ibada hiyo na kumsindikiza ndugu yake, akimwomba Mungu ampe faraja, nguvu na kumlinda katika kipindi hiki kigumu, huku akiomba pia Mungu aifariji familia yote.

Jambo TV
Jambo TV
Open In TikTok:
Region: TZ
Sunday 08 November 2026 15:55:46 GMT
8956
455
9
6

Music

Download

Comments

sumbawangq4
Mbalalahome :
Sahii yatakwisha
2026-11-08 16:44:06
2
jinakubwa1900
BeautfulTANZANIA :
Mungu azidi kumpa Nguvu Tundu Lissu huko Gerezani
2026-11-08 16:40:39
2
amos.saimon5
Amos Saimon :
Lissu the hero of afrika
2026-11-08 17:01:21
0
itslazar6
Baba D Madini 💶💴💎🚙 :
Hii inauzunisha sana jaman
2026-11-08 16:43:01
1
treasures.mushi
Treasures Mushi :
Mungu amtie nguv katik kipnd hk kigum,
2026-11-08 17:13:58
0
nelly.sylvester4
Nelly Sylvester :
Mungu ni wetu sote
2026-11-08 17:24:32
0
omujinite.com96
big joe :
Mungu atajibu Kwa wakati unaofaa
2026-11-08 17:03:01
0
aronfrank76
Aronfrank :
mungu yupoo
2026-11-08 17:14:08
0
user207376997887
mama ese :
apumzike kwa amani
2026-11-08 17:11:32
0
kobe79412
lokii :
kuna vitu vinaumiza sana kama ww ni binadamu
2026-11-08 16:40:13
1
petroalfred
petroalfred :
Nchi inaongozwa na mashetani wanyonya damu
2026-11-08 17:14:11
0
ambokile.paschal6
Ambokile Paschal :
🙏🙏🙏
2026-11-08 16:38:47
1
juliusmnikomtundi
juliusmnikomtundi :
🙏🙏🙏
2026-11-08 16:44:42
1
elisha81555
ELA DADA :
🥰🥰🥰
2026-11-08 17:19:16
0
To see more videos from user @jambotv_, please go to the Tikwm homepage.

Other Videos


About