@cawabemedia_: Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba, amekemea vikali vitendo vya urasimu, uzembe na ubinafsi vinavyofanywa na baadhi ya watumishi katika sekta ya afya nchini, akisisitiza kuwa serikali haitakubali taratibu za kiutendaji kutumika kama sababu ya kuchelewesha huduma kwa wagonjwa. Dkt. Mwigulu amesema kuwa hakuna sababu ya msingi inayoweza kuhalalisha mgonjwa kunyimwa au kucheleweshewa huduma ya afya kwa kisingizio cha kukosekana kwa vifaa vidogo, akitolea mfano wa akina mama wajawazito wanaofika hospitalini wakiwa katika hatua ya uchungu lakini badala ya kuhudumiwa haraka, wanaanza kuulizwa vifaa kama beseni. Amesisitiza kuwa maisha ya mwananchi yanapaswa kupewa kipaumbele kuliko taratibu zisizo za lazima, akiwataka wataalamu wa afya kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia utu, huruma na dhamana waliyonayo ya kuokoa maisha ya watu. Kauli hiyo ameitoa wakati akizungumza na wananchi katika viwanja vya Stendi ya Mwanhuzi, Kijiji cha Bomani, wilayani Meatu mkoani Simiyu. Amesema serikali haiwezi kukubali uzembe na ubinafsi wa baadhi ya watumishi kugeuzwa kuwa utaratibu wa kawaida katika utoaji wa huduma za afya, hasa pale ambapo ucheleweshaji wa huduma unaweza kuhatarisha maisha ya wagonjwa. Aidha, amewataka watumishi wa sekta ya afya kujitathmini na kuhakikisha wanatoa huduma kwa wakati bila kuweka vikwazo visivyo vya lazima, akisisitiza kuwa wito wao mkubwa ni kuwahudumia wananchi na kulinda maisha yao. Ameeleza kuwa ni muhimu kila mtumishi wa afya kutambua kuwa mgonjwa anayefika hospitalini anahitaji msaada, hivyo anapaswa kupokelewa na kuhudumiwa kwa haraka na kwa utu bila kujali hali yake ya kiuchumi au mazingira aliyotoka.

cawabemedia
cawabemedia
Open In TikTok:
Region: TZ
Monday 09 November 2026 06:00:19 GMT
39820
1495
94
61

Music

Download

Comments

halima.juma045
Mrs muuu0755 :
mm niljifunguwa kwa upareshen sikunaenda kusafsha kidonda niliobwa ela saiv kutbiwa bule hakupo mweshimiwa
2026-11-10 03:12:14
1
zainashehoza
Zaina Shehoza :
nazaaa tena ngj nitege mimba nahii clipu naenda nayo cku ya.kuzaa
2026-11-10 05:07:18
1
user4923675307881
Eliza :
Baba acha tu tukienda hospital tunanyanyasika sana hasa mama wenye uchungu wa kujifungua, na hospital zingine ukijifungua mtoto wa kiume unalipia hela kubwa wa kike hela kidg sasa hapo nashindwa kuelewa jmn
2026-11-10 04:16:48
2
annastaziafausti71
Annastazia :
nikwer unatutetea lakini je,watatekeleza maana wao kunyanyasa watu ndo sifa yao
2026-11-10 05:41:49
1
user958143293612
beatrice :
baba mungu akupe maishamalefu mnooooo lispect you baba tumechoshwa nauzembe hospitali za Tz
2026-11-10 05:10:15
1
remi.fanicha.0745003670
REMI [ mtaalam wa fanicha :
watu mikoani wanakufa wakiwa wanachati
2026-11-09 17:22:39
6
ludovicaraphael
ludovicaraphael :
MUHESHIMIWA MBONA KILAMAHALI WATOTO CHINI YA MIAKA MITANO MPAKA WACHANGA KABISA TUNALIPIA??
2026-11-09 19:17:30
1
maydaabdul0
madam~mayda💞💦 :
hosptal nyingine hta cheti cha kizaliwa unaombwa hela ya bando🤣🤣
2026-11-10 04:26:30
0
user8723655706735
msiziloofficial :
tunashukuru sana
2026-11-10 04:38:56
1
sophynyirendagmail
[email protected] :
wewe unasema , kutekeleza ndo issue
2026-11-10 04:58:26
1
annastazia.annast49
AN :
iyo lini iyoooo
2026-11-10 01:34:59
1
user91753665421695
pilly :
kwel baba tunateseka sana upewi uduma eti lete kalatasi janani mara kakate fairi jamani mtu unaumwa uchungu😳😳😳
2026-11-10 05:53:36
0
user930717628
Halima :
baba umeongey ukweli
2026-11-09 19:50:19
1
chiddisalum
chiddisalum :
jamani tuliyani tunateseka bilaela unafiya mapokezi
2026-11-10 05:08:31
0
user8463552828397
Jam🌹 :
waziri tunae na tunatamba nae
2026-11-09 06:15:01
1
user41953745217775
user41953745217775 :
kabisa baba wajawazito tunateseka unaenda hujaziw kadi kwawakati ikizidiwa unaitwa mpaka mwisho mpaka waje watusaidie umeshachoka asante baba mtetezi wetu
2026-11-09 22:14:33
0
marry.jonasy
Marry Jonasy :
Asantee baba mungu akubaliki sana
2026-11-09 22:00:11
0
marunde43
Nuru Akida :
maneno ya kwenye majukwaa hayoo ukifika hospital wahudumu wanakuulia mgonjwa wakoo
2026-11-09 08:30:40
0
user6948319922904
Agness Gerald :
sema sana baba pokea maua yako
2026-11-10 05:50:10
0
reyra211
Reyra😋 :
Mimi niliambiwa una BEI GANI TUKUSAIDIEEEEE BABAAAAAA
2026-11-10 05:59:44
0
sabasabatrespholy
Saba saba Trespholy :
mzeeeeeeeee umesema
2026-11-10 05:59:04
0
user73732739983
Humble :
SAHIHI BABA
2026-11-10 06:02:52
0
caristajoseph
MRS SANGA🫂♥️🥰 :
Baba kadi tunafungua na pesa na kliniki bila pesa hatubembei
2026-11-10 05:58:00
0
user2632957838127
edwina :
asante baba, meseng send but kazia baba kazia
2026-11-10 05:56:04
0
happyfania622
Happy :
hizo ni stories hivi unawajua vizuri wauguzi wakiharibu wanateteana pesa mbele
2026-11-09 08:46:43
0
To see more videos from user @cawabemedia_, please go to the Tikwm homepage.

Other Videos


About