Naitwa Baba Travis :
Kama Unataka kuokoka na kutegua kitendawili cha utatu Mtakatifu soma hapa !!! Yesu Kristo ni Mungu 100%. Yeye ni Neno la Mungu ambaye kupitia yeye vitu vyote viliumbwa. Yeye ndiye njia ya wokovu na uzima wa milele.
Baada ya Adamu kuanguka dhambini, dhambi iliingia ulimwenguni, mwanadamu akapoteza utukufu wa Mungu na kuwa chini ya utawala wa dhambi na mauti. Kupitia anguko hilo, Shetani akapata nafasi ya kumtawala mwanadamu. Ndipo ilipohitajika Neno la Mungu, ambaye ndiye mwanzo wa vitu vyote, kufanyika mwili kwa uweza wa Mungu ili kumkomboa mwanadamu na kurejesha kile kilichopotea.
Mungu alisuka mpango wake wa wokovu kupitia Ibrahimu na taifa la Israeli, hadi wakati ulipotimia Kristo akaja. Yesu alikufa msalabani, akalipa gharama ya dhambi na kutukomboa kutoka katika utumwa wa dhambi na mauti. Kumwamini na kumfuata Kristo ni kutoka katika ufalme wa giza na kuingia katika ufalme wa Mungu, tukipokea uzima wa milele.
Mungu ni mmoja. Tunapozungumzia Utatu Mtakatifu, tunamaanisha Mungu mmoja katika nafsi tatu: Baba, Mwana na Roho Mtakatifu, si miungu watatu. Yesu Kristo ndiye ufunuo kamili wa Mungu kwa mwanadamu.
Tuchukulie mfano wa mwanadamu. Rais Samia ni mtu mmoja, lakini kwa wakati mmoja anashika Tatu nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu. Na Mwenye kiti wa chama chake nafasi Zote hizo bado ni Katika Mamlaka yake ya URais Mfano huu unatupa picha ya kuelewa kwamba mambo yanayohusiana na Mungu yanaweza kuzidi namna tunavyoyafikiria kwa akili zetu. Hata hivyo, huu ni mfano wa kufafanua tu; Utatu Mtakatifu si Mungu mmoja anayebadilisha nafasi au kuvaa sura tofauti, bali ni Mungu mmoja katika nafsi tatu: Baba, Mwana na Roho Mtakatifu.
Usipime uweza wa Mungu kwa akili na mantiki ya kibinadamu. Mungu hafungwi na nafasi, muda wala mahali. Kujidhihirisha kwake katika mwili kupitia Yesu Kristo hakumaanishi kwamba uwepo wake wote ulifungiwa duniani.
Roho Mtakatifu ni Mungu, anakaa ndani ya waamini, akiwaongoza, akiwatia nguvu katika udhaifu wao na kuwasaidia kushinda majaribu na nguvu za yule mwovu.
2026-11-09 19:22:00