@mgodiwaafya: MAMBO 5 YA KUZINGATIA WAKATI WA KUTAFUTA UJAUZITO ☑️ 01. Tumia Folic Acid Kila Siku: Tumia Folic Acid 400 mcg kila siku kabla ya kupata ujauzito ili kusaidia ukuaji wa awali wa mtoto na kuzuia kasoro za mfumo wa fahamu. ☑️ 02. Kula Lishe Bora: Hakikisha unakula vyakula vyenye mboga za majani, matunda, protini na nafaka zisizokobolewa ili kuupa mwili virutubisho muhimu. ☑️ 03. Punguza Sukari Na Vyakula Vilivyosindikwa: Epuka ulaji wa sukari nyingi, vyakula vya viwandani na vyakula vyenye mafuta mengi yasiyo na afya. ☑️ 04. Kunywa Maji Na Kufanya Mazoezi: Kunywa maji ya kutosha kila siku na kufanya mazoezi ya wastani ili kudumisha afya njema ya mwili. ☑️ 05. Mshirikishe Mwenza Wako: Hakikisha mwenza wako pia anazingatia lishe bora na mtindo mzuri wa maisha kwa ajili ya kusaidia afya ya mbegu za kiume. KUMBUKA:Kuitwa mama sio kitu chepesi ivo ni jambo la kipekee sana,na kuna mda linakuja na Changamoto zake zinatokana na vitu mbalimbali ambavyo baadhi unawezakua ulisababisha mwenyewe au ulisababishiwa,ivyo uonapo ugumu usisite kuomba ushauri 0718639776 tupo wasap na kawaida. Like,Share,Comment And Follow #mgodi_wa_afya #uzazieden #wanawake